-
Rais wa Tunisia avunja Baraza Kuu la Idara ya Mahakama
Feb 07, 2022 02:31Rais Kais Saied wa Tunisia ametangaza habari ya kulivunja Baraza Kuu la Idara ya Mahakama, huku msuguano mkali ukiendelea kushuhudiwa baina yake na mhimili huo wa dola.
-
Umoja wa Mataifa waelezea kusikitishwa na hali mbaya ya kisiasa nchini Tunisia
Jan 22, 2022 14:04Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kufuatia kuongezeka ukandamizaji wa wapinzani nchini Tunisia sambamba na wakati huu wa kuadhimisha mapinduzi ya wananchi yaliyomng'oa madarakani dikteta Zainul Abidin Ben Ali.
-
Chama cha Nahdha Tunisia chataka kuhitimishwa ukandamizaji dhidi ya waandamanaji
Jan 16, 2022 02:45Chama cha Nahdha cha Tunisia kimetoa taarifa kikitaka kuhitimishwa vitendo vya utumiaji mabavu na ukandamizaji unaofanywa na vikosi vya usalama dhidi ya maandamano ya amani ya wananchi wa nchi hiyo.
-
Rais wa Tunisia akosolewa kwa kuandaa bajeti bila kumshirikisha yeyote
Jan 15, 2022 11:09Muungano wa Wafanyakazi Tunisia (UGTT) umemkosoa vikali Rais Kais Saied wa nchi hiyo, kwa kutwaa mamlaka yote ya nchi, na kuandaa bajeti ya nchi yeye binafsi pasi na kuzishirikisha taasisi nyingine husika.
-
Maandamano dhidi ya serikali nchini Tunisia katika maadhimisho ya mapinduzi ya Januari 14
Jan 15, 2022 10:41Sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa 11 wa harakati ya wananchi wa Tunisia iliyopelekea kupinduliwa serikali ya dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Zine El Abidine Ben Ali, Tunisia jana Ijumaa ilishuhidia maandamano makubwa ya kupinga utendaji wa kiongozi wa sasa wa nchji hiyo, Kais Saied.
-
Chama cha Ennahda Tunisia chatoa wito wa maandamano makubwa Ijumaa ijayo
Jan 11, 2022 14:10Chama cha Ennahda chenye mfungamano na Harakati ya Ikhwanul Muslimini cha Tunisia kimetoa taarifa kikiwatolea wito wananchi kushiriki kwa wingi katika maandamano yatakayofanyika nchini humo Ijumaa tarehe 14 mwezi huu wa Januari.
-
Spika wa Bunge, Mawaziri Wakuu wa zamani wa Tunisia kupandishwa kizimbani
Jan 08, 2022 02:49Spika wa bunge lililovunjwa la Tunisia na Mawaziri Wakuu wa zamani wa nchi hiyo watafikishwa kizimbani kwa tuhuma za kukiuka sheria za kampeni za kisiasa na kutobainisha vyanzo vya fedha zao wakati wa kampeni za uchaguzi.
-
Spika wa bunge lililovunjwa na waziri mkuu wa zamani wa Tunisia wafunguliwa mashtaka
Jan 06, 2022 07:56Spika wa Bunge lililovunjwa na waziri mkuu wa zamani wa Tunisia watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukiuka sheria za uendeshaji kampeni za kisiasa na kutobainisha wazi vyanzo vya fedha walizotumia katika kampeni za uchaguzi.
-
Miito yatolewa Tunisia kwa ajili ya kuachiwa huru Naibu Mkuu wa Annahdha
Jan 03, 2022 02:35Miito imeendelea kutolewa nchini Tunisia ili kuachiwa huru mwanasiasa aliyeko kizuini, Noureddine Bhiri, ambaye pia ni Naibu Mkuu wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa huko Tunisia cha Annahdha.
-
Afisa mwandamizi wa Annahdha 'atekwa nyara' na maafisa usalama Tunisia
Jan 01, 2022 12:34Harakati ya Annahdha nchini Tunisia imesema kuwa, afisa mwandamizi wa chama hicho cha kisiasa ametiwa mbaroni na maafisa usalama wa nchi hiyo.