-
Rais wa Ufaransa na viongozi kadhaa wa Afrika wahudhuria mazishi ya Rais Deby wa Chad
Apr 23, 2021 22:50Mazishi ya rais Idriss Deby wa Chad yalifanyika jana Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo N'Djamena, ambapo maelfu ya watu walitoa heshima zao wa mwisho wa kiongozi huyo aliyefariki kutokana na majeraha aliyopata katika mstari wa mbele wa vita wakati akiongoza jeshi lake kukabiliana na shambulio la waasi.
-
Watu wasiopungua 21 wafariki baharini baada ya boti kuzama katika pwani ya Tunisia
Apr 16, 2021 22:13Watu wasiopungua 21 wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wameabiri kuzama katika pwani ya Tunisia wakati wakijaribu kuvuka maji ya bahari ya Mediterania ili kufika kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.
-
Rais wa Tunisia apinga kufanyiwa marekebisho Mahakama ya Katiba
Apr 04, 2021 23:58Rais wa Tunisia amemtumia ujumbe Spika wa Bunge la nchi hiyo akipinga kufanyiwa marekebisho Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo.
-
Chama cha al Nahdha chahimiza kuanza mazungumzo ya kitaifa nchini Tunisia
Apr 02, 2021 02:05Chama cha Kiislamu cha al Nahdha nchini Tunisia kimetangaza kuwa, kuna wajibu kwa wanasiasa kuanzisha mazungumzo ya kitaifa ili kupunguza mivutano katika nyuga tofauti za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Watunisia waungana na Wapalestina kuadhimisha Siku ya Ardhi na kulaani kuanzisha uhusiano na Israel
Mar 31, 2021 07:19Jumuiya na makundi mbali mbali ya kisiasa na kiraia nchini Tunisia yameadhimisha Siku ya Ardhi ya Palestina na kulaani juhudi na hatua zozote zile za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Wananchi wa Tunisia waendelea na maandamano ya kulalamikia mgogoro wa kisiasa
Mar 21, 2021 08:55Wananchi wa Tunisia wameendelea na maandamano ya kupinga mgogoro wa kisiasa na matatizo ya kiuchumi na kimaisha nchini mwao.
-
Spika wa Bunge la Tunisia amkosoa Rais kwa kutotoa idhini kwa mawaziri kula kiapo
Mar 11, 2021 03:47Spika wa Bunge la Tunisia Rached Ghannouchi amekosoa hatua ya Rais Kais Saied wa nchi hiyo ya kutowapa idhini mawaziri walioteuliwa katika serikali mpya kula kiapo.
-
Maelfu ya wananchi wa Tunisia waandamana mjini Tunis kuiunga mkono serikali
Feb 28, 2021 04:32Maelfu ya wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano kufuatia mwaliko wa chama tawala cha An Nahdhah na kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya nchi hiyo.
-
Waziri Mkuu wa Tunisia awapiga kalamu nyekundu mawaziri 5
Feb 15, 2021 23:14Waziri Mkuu wa Tunisia amewafuta kazi mawaziri watano katika baraza la mawaziri la nchi hiyo na kuwateuwa wengine kushika nyadhifa hizo.
-
Watunisia waandamana wakipinga kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel
Feb 15, 2021 06:59Wananchi waliokuwa na hasira wa Tunisia wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis, wakipinga hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.