Watunisia waandamana wakipinga kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66882-watunisia_waandamana_wakipinga_kuanzishwa_uhusiano_na_utawala_wa_kizayuni_wa_israel
Wananchi waliokuwa na hasira wa Tunisia wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis, wakipinga hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 15, 2021 06:59 UTC
  • Watunisia waandamana wakipinga kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel

Wananchi waliokuwa na hasira wa Tunisia wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis, wakipinga hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao wamekusanyika mbele ya jengo la ubalozi wa Ufaransa mjini Tunis na kutoa nara zinazolaani kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni.

Wananchi hao wa Tunisia wamelaani usaliti huo wa baadhi ya nchi za Kiarabu na wamezitaka nchi za Kiislamu kufanya harakati ya kutetea kadhia nambari moja ya Umma wa Kiislamu yaani kadhia ya Palestina. 

Vilevile wamepinga vikali uingiliaji wa Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi yao na kutoa wito wa kuachiwa huru Georges Ibrahim Abdallah, raia wa Lebanon anayeshikiliwa jela nchini Ufaransa na vilevile Ahmad Saadat ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Kipaletina wanaoshikiliwa katika jela ya utawala haramu wa Israel.

Waandamaji wa Tunisia wapinga uhusiano na Israel

Nchi za Tunisia na Algeria zimekataa kuruhusu ndege ya utawala ghasibu wa Israel kupita katika anga yao baada ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo na pande hizo mbili kukubaliana kuanza safari za ndege za Israel nchini Morocco.