Maelfu ya wananchi wa Tunisia waandamana mjini Tunis kuiunga mkono serikali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i67352-maelfu_ya_wananchi_wa_tunisia_waandamana_mjini_tunis_kuiunga_mkono_serikali
Maelfu ya wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano kufuatia mwaliko wa chama tawala cha An Nahdhah na kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2021 04:32 UTC
  • Maelfu ya wananchi wa Tunisia waandamana mjini Tunis kuiunga mkono serikali

Maelfu ya wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano kufuatia mwaliko wa chama tawala cha An Nahdhah na kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya nchi hiyo.

Huku wakipiga nara ya "wananchi wa Tunisia wanataka umoja wa kitaifa", wafanya maandamano hao wametaka makundi ya kisiasa nchini humo kuheshimu demokrasia na katiba ya nchi. 

Rashid al Ghanoush Mkuu wa chama cha An Nahdhah na ambaye pia ni Spika wa bunge la Tunisia amekosoa hatua ya Rais Kais Saeid wa nchi hiyo ya kupinga kutekelezwa mabadiliko ndani ya serikali na kutaka kufanyika mazungumzo ya kitaifa na kuunga makundi ya kisiasa huko Tunisia.   

Rashid al Ghanoush, Mkuu wa chama tawala cha An Nahdhah cha Tunisia 

Rais wa Tunisia anaamini kuwa, mabadiliko yaliyofanywa katika baraza la mawaziri ni kinyume cha sheria. Amesema kuna uwezekano wa kuwepo ufisadi na mgongano wa kimaslahi baina ya mawaziri. 

Hichem al Mechichi Waziri Mkuu wa Tunisia tarehe 16 mwezi Januari mwaka huu alilifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri; ambapo aliwateuwa mawaziri 11 kutoka vyama vinavyoiunga mkono serikali. 

Hii ni katika hali ambayo, tangu wakati huo hadi sasa Rais Kais Saeid wa Tunisia bado hajawaalika katika ikulu ya Qartaj mawaziri hao walioteuliwa ili kuapishwa.