Jul 29, 2023 03:36
Karibu watu mashuhuri 800 wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wametangaza mshikamano wao na Spika wa Bunge lililovunjwa la Tunisia, Rached Ghannouchi, kwa mnasaba wa kutimia siku 100 tangu kukamatwa kwake, na wametoa wito wa kuachiwa huru wafungwa wote wa kisiasa nchini Tunisia bila masharti yoyote.