-
Magaidi wa Al Shabab waua afisa wa utawala Kenya
May 16, 2017 09:43Watu wanaoaminika kuwa magaidi wa kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia wameingia katika eneo la mpakani kaskazini mashariki mwa Kenya na kumuua afisa mmoja wa utawala nchini humo.
-
UN: Ubakaji unatumiwa kama mbinu ya ugaidi Somalia, Nigeria
May 16, 2017 09:14Umoja wa Mataifa umesema uhalifu wa kijinsia unatumiwa na magaidi kama moja ya mbinu zao katika nchi za Somalia, Nigeria na Mali.
-
Iran yakamata magaidi na kunasa mada za milipuko
May 13, 2017 09:27Vikosi vya usalama Iran vimefanikiwa kusambaratisha kijikundi cha kigaidi ambacho kilikuwa kinapanga kutekeleza hujuma ndani ya nchi.
-
Rais wa Somalia aomba msaada wa kimataifa
May 11, 2017 23:12Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia ameiuomba jamii ya kimataifa iisaidie nchi yake katika kupambana na ugaidi, ufisadi na umaskini wa kuchupa mipaka; mambo ambayo amesema ndiye adui mkuu wa nchi hiyo.
-
Sisitizo la Putin la kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi, misimamo mikali na unazi mambo leo
May 10, 2017 00:54Rais Vladimir Putin wa Russia alisema katika hotuba aliyoitoa jana Jumanne kwa mnasaba wa Siku ya Ushindi mjini Moscow kwamba kuna udharura kwa jamii ya kimataifa kusimama imara na kushirikiana kukabiliana na vitisho vinavyohatarisha usalama wa wote. Amesema, kuna udharura wa kuweko mapambano ya kweli dhidi ya ugaidi, misimamo mikali, unazi mambo leo na kila kitu kinachohatarisha usalama wa kimataifa. Aidha amesema, Moscow iko tayari kushirikiana na nchi yoyote ile katika jambo hilo.
-
Iran: Kauli ya Salman ni ithibati kuwa Saudia inaunga mkono ugaidi
May 03, 2017 23:33Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia ni dhihirisho tosha kuwa Riyadh inaunga mkono ugaidi na utawala huo wa kifalme umejengeka katika misingi ya sera haribifu.
-
Hatari ya ugaidi, changamoto kubwa zaidi ya Misri
May 01, 2017 23:55Rais Abdulfattah as-Sisi, wa Misri amesema kwamba hatari ya ugaidi ni changamoto kubwa zaidi kati ya changamoto zinazoikabili nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Putin asisitiza udharura wa kuwepo msimamo mmoja katika kupambana na ugaidi
Apr 27, 2017 21:58Rais Vladmi Putin wa Russia amesema katika ujumbe uliosomwa kwenye Mkutano wa Sita wa Usalama wa Kimataifa mjini Moscow kwamba, mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika yanahitaji kuwa na mtazamo na msimamo mmoja na unaooana.
-
Nchi za magharibi mwa Afrika zakutana na kujadili namna ya kupambana na ugaidi
Apr 27, 2017 23:14Watalaamu kutoka nchi 10 za magharibi mwa Afrika wamekutana katika mji mkuu wa Togo, Lome na kujadili namna ya kupambana na tatizo la ugaidi pamoja na njia za kuboresha usalama na amani katika ndege za abiria.
-
Zarif atoa wito wa kupambana na ugaidi na misimamo ya kuchupa mipaka
Apr 27, 2017 03:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jitihada za pamoja za kimataifa zinahitajika ili kung'oa mizizi ya ugaidi na kuenea wimbi la misimamo mikali ya kufurutu ada.