Iran yakamata magaidi na kunasa mada za milipuko
Vikosi vya usalama Iran vimefanikiwa kusambaratisha kijikundi cha kigaidi ambacho kilikuwa kinapanga kutekeleza hujuma ndani ya nchi.
Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumamosi ilitangaza kufanikiwa kuzima njama za kijikundi kimoja cha kigaidi katika oparesheni maalumu ya vikosi vya usalama.
Taarifa hiyo imesema kijikundi hicho cha kigaidi huko nyuma kiliwahi kuhusika na mauaji ya maelfu ya watu wasio na hatia Iran. Aidha kundi hilo la kigaidi limekuwa likishirkiana na madola adui katika kutekeleza ujasusi ndani ya nchi. Kwa mujibu wa Wizara ya Usalama ya Iran, magaidi hao pia wamekamatwa wakiwa na mada za milipuko.
Taaria hiyo aidha imesema kundi hilo la kigaidi linapanga kuwatumia watu wasio na uelewa ili watekekeza vitendo vya kigaidi na hujuma nyinginezo haribifu na kwa msingi huo wananchi Wairani wametakiwa kuwa macho kuhusu njama hizo.
Mwezi Februari, Waziri wa Usalama Iran Sayyed Mahmoud Alawi alisema vikosi vya usalama nchini vilifanikiwa kuwakamata watu 8 ambao wanafungamana na makundi ya magaidi wakufurishaji waliokuwa wamepanga kutekeleza hujuma za kigaidi hapa nchini.