-
Kenyatta amualika Odinga katika sherehe za kuapishwa kwake
Nov 25, 2017 04:22Rais Uhuru Kenyatta amemualika 'ndugu yake' Raila Odinga katika sherehe za kuapishwa kwake zikatazofanyika katika mji mkuu Nairobi Jumanne ijayo ya Novemba 28.
-
Jeshi Kenya laua waandamanaji watatu, magari kadhaa yachomwa, Raila arejea nchini
Nov 17, 2017 16:50Watu watatu wameuawa hii leo wakati jeshi la polisi la Kenya lilipojaribu kutawanya waandamanaji waliokusanyika kupokea msafara wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga aliyerejea nchini mapema leo akitokea nje ya nchi.
-
Uhuru Kenyatta atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi wa rais Kenya uliosusiwa na mpinzani wake
Oct 30, 2017 16:22Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya IEBC Wafula Chebukati amemtangaza Uhuru Kenyatta, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Jubilee Rais mteule na mgombea wake mwenza William Ruto kuwa Naibu Rais mteule baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa marudio wa rais uliofanyika siku ya Alkhamisi.
-
Ruto: Uchaguzi mwingine Kenya utafanyika 2022, wala sio ndani ya siku 90
Oct 30, 2017 08:04Naibu wa Rais wa Kenya amesema uchaguzi mwingine wa rais utafanyika mwaka 2022 kwa mujibu ya miongozo ya Katiba na Sheria za Uchaguzi na wala sio ndani ya siku 90 kama anavyoshinikiza kinara wa upinzani nchini humo Raila Odinga.
-
Uhuru Kenyatta aongoza kwa 96%, Odinga ataka uchaguzi mpya ndani ya siku 90
Oct 28, 2017 09:44Rais Uhuru Kenyatta anaongoza kwa asilimia 96 katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika Alkhamisi iliyopita nchini Kenya.
-
UN na AU zatoa wito wa amani kabla ya uchaguzi wa marudio Kenya
Oct 23, 2017 13:54Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zimetoa taarifa ya pamoja zikitoa wito kwa wanasiasa na polisi nchini Kenya kuzingatia sheria katika kutatua mgogoro uliopo nchini humo.
-
Kenya kukabiliana na maandamano ya wapinzani
Sep 29, 2017 14:38Serikali ya Kenya imesema maandamano ya muungano wa upinzani Nasa ambayo yamepangwa kuanza Jumatatu yatadhibitiwa na vitengo vya kuimarisha usalama vya nchi hiyo.
-
Polisi Kenya watawanya wapinzani wanaotaka mabadiliko tume ya uchaguzi
Sep 26, 2017 16:06Polisi wa kuzima ghasia nchini Kenya wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakitaka baadhi ya maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC wafutwe kazi kabla ya uchaguzi wa rais wa marudio wa Oktoba 26.
-
Rais wa Kenya: Hukumu ya Mahakama ya Juu ilikuwa ni "mapinduzi"
Sep 21, 2017 15:45Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema Mahakama ya Juu ya nchi hiyo ilifanya "mapinduzi" dhidi ya matakwa ya wananchi ilipobatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita ambao yeye alishinda.
-
Wafuasi wa Jubilee waandamana Kenya kupinga uamuzi wa Mahakama
Sep 19, 2017 15:53Polisi nchini Kenya wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta ambao walikuwa wakiandamana nje ya Mahakama ya Kilele mjini Nairobi wakipinga uamuzi wa mahakama hiyo kubatilisha uchaguzi wa rais wa Agosti 8.