-
Iran: Tuna hamu kubwa ya kustawisha uhusiano na nchi za eneo letu kadiri inavyowezekana
Jan 05, 2019 03:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina hamu kubwa ya kustawisha uhusiano wake na majirani zake na nchi nyingine za eneo hili kadiri inavyowezekana kupitia ushirikiano, kupandisha juu kiwango cha uhusiano na kupunguza hitilafu zilizopo.
-
Mogherini: EU haitairuhusu Marekani iingilie uhusiano wake na Iran
Jan 02, 2019 15:17Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema Marekani haiwezi na haipaswi kuitwisha EU sera zake na kwamba umoja huo wenye nchi wanachama 28 hautairuhusu Washington iufanyie maamuzi juu ya uhusiano wake wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Hadashot TV: Israel na Saudia kutangaza rasmi uhusiano wao ndani miezi michache ijayo
Dec 09, 2018 07:24Kanali mashuhuri ya televisheni ya Hadashot ya utawala haramu wa Israel imefichua kuwa, Tel Aviv ipo mbioni kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Saudi Arabia, na kwamba uhusiano wa tawala mbili hizo utafanywa wa kawaida na rasmi ndani ya miezi michache ijayo.
-
Rwanda yasisitiza kuimarisha uhusiano na Iran
Nov 15, 2018 03:32Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Richard Sezibera amepongeza uhusiano mzuri wa pande mbili kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitizia umuhimu wa kupanuliwa uhusiano huo katika nyuga mbalimbali.
-
Uganda na Iran kuimarisha ushirikiano katika uga wa sayansi na teknolojia
Oct 05, 2018 15:38Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Uganda ametoa mwito wa kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa sayansi na teknolojia.
-
Rais Rouhani wa Iran amtumia salamu Rais Kabila wa DRC
Jul 01, 2018 13:55Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtumia salamu za pongezi Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa munasaba wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi hiyo.
-
Sudan yalalamikia udhalilishaji wa Misri
May 21, 2018 02:34Uhusiano baina ya Misri na Sudan umezidi kuharibika baada ya Khartoum kuilalamikia Cairo kuwa inafanya udhalilishaji dhidi yaWamisri waishio nchini Sudan.
-
Saudia yaanza duru mpya ya kuwakamata wale wanaopinga nchi hiyo kuwa na uhusiano na Israel
May 20, 2018 02:22Vyombo vya habari, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wameelezea kupitia mitandao ya kijamii juu ya kuanza duru mpya ya kamatakamata ya utawala wa kifalme wa Aal-Saud dhidi ya wapinzani wanaopinga nchi hiyo kuwa na uhusiano na utawala katili wa Kizayuni.
-
Kuimarika uhusiano wa Zimbabwe na China
Apr 05, 2018 01:39Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amemshukuru rais mwenzake wa China Xi Jinping kwa uungaji mkono wa kisiasa wa nchi hiyo kwa Zimbabwe na kutaka kuimarishwa zaidi uhusiano wa pande mbili.
-
Iran na Oman zasisitizia ulazima wa kuimarishwa amani na uthabiti katika eneo
Mar 18, 2018 16:49Rais Hassan Rouhani amesisitiza juu ya kuimarishwa na kustawishwa zaidi uhusiano uliopo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman.