May 12, 2020 14:43
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, huenda vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi katika nchi za chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika vikaongezeka mara mbili, iwapo jitihada za kiafya za kuwashughulikia wenye virusi vya HIV zitakatizwa na janga la kimataifa la corona.