Aug 17, 2017 04:11 UTC
  • Rais Lungu asema ni lazima kupimwa HIV/UKIMWI nchini Zambia

Rais Edgar Lungu wa Zambia amesema sasa ni lazima wananchi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kufanyiwa vipimo vya virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Ukimwi, ikiwa ni katika jitihada za taifa hilo kulitokomeza jinamizi hilo kikamilifu kufikia mwaka 2030.

Lungu aliyasema hayo katika mji mkuu Lusaka, wakati wa uzinduzi wa 'Siku ya Kupimwa HIV, Ushauri-Nasaha na Matibabu' chini ya kaulmbiu "Pima na Tibu".

Rais wa Zambia amesema agizo la kufanyiwa vipimo vya HIV sasa ni lazima na hakuna mjadala kuhusu sera hiyo mpya ya serikali; na kuhoji kuwa wanaopiga makele kwamba agizo hilo linakiuka haki za binadamu, mbona wanakimya wakati mwenye Ukimwi anaambukiza na kuua wenzake?  

Kibango cha kuhamasisha umuhimu wa kupimwa HIV

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO,  karibu nusu ya watu wanaoishi na virusi vya HIV kote duniani sawa na watu milioni 14, hawajafanyiwa vipimo kutambua iwapo wameambukizwa virusi hivyo hatari vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi au la.

Aidha Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF hivi karubuni ulisema kuwa, virusi vya HIV na ugonjwa hatari wa UKIMWI vingali sababu kuu ya vifo vya vijana wenye umri wa kati ya miaka 10-19 barani Afrika, licha ya jitihada za kimataifa za kukabiliana nao.

Asilimia 70 ya watu wanaoishi na ugonjwa huo duniani ni vijana kutoka eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika.

Tags