-
Takwa la Ujerumani la kuasisiwa Baraza la Usalama la Umoja wa Ulaya
Oct 10, 2018 04:29Kuibuka hitilafu na mizozo mikubwa baina ya Marekani na Umoja wa Ulaya baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump hususan katika masuala ya kiulinzi, nafasi na umuhimu wa Shirika la Kijeshi la NATO sambamba na kujitoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya (Brics) ni mambo ambayo yamezifanya nchi wanachama wa EU zichukue hatua za kuimarisha mipango na mikakati ya kujitegemea katika uga wa ulinzi na usalama.
-
Ufaransa: Marekani haina haki ya kuchukua maamuzi kwa niaba ya Ulaya
Oct 06, 2018 03:46Waziri wa Fedha wa Ufaransa amesema kuwa, Marekani haiwezi kuchukua maamuzi kuhusiana na ushirikiano wa kibiashara wa nchi za Ulaya na Iran na kuongeza kuwa, vikwazo vya serikali ya Washington dhidi ya Iran ni fursa kwa Ulaya kwa ajili ya kuanzisha taasisi zinazojitegemea za kifedha.
-
Qassemi: Msimamo wa Ulaya unakidhi maslahi ya Iran katika JCPOA
Oct 01, 2018 11:17Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumekuwa na hali ya kukaribiana misimamo ya Iran na Ulaya kuhusiana na kukidhiwa maslahi ya Tehran baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi.
-
Zarif: Ikiwa utaratibu uliowekwa na Ulaya hautotekelezeka, Iran itajitoa kwenye JCPOA
Sep 30, 2018 04:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, ikiwa utaratibu maalumu ulioratibiwa na Ulaya kwa ajili ya kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hautakuwa na ufanisi wa utekelezaji, Iran itajitoa kwenye makubaliano hayo.
-
Ushauri wa Trump kwa Ulaya: Jengeni ukuta wa kizuizi eneo la Afrika la Jangwa la Sahara
Sep 21, 2018 02:58Vyombo vya habari vya Uhispania vimefichua kuwa rais wa Marekani amezishauri nchi za Ulaya zitumie mbinu ya kujenga ukuta wa kizuizi kukabiliana na wahajiri kutoka Afrika.
-
Indhari kuhusu safari za wahajiri kuelekea Ulaya zenye kuhatarisha maisha
Sep 03, 2018 09:01Mjumbe Maalumu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa katika kituo cha Mediterania ametahadharisha kuwa wahajiri hukabiliana na hatari chungu nzima wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kufika Ulaya.
-
Qassemi: Hatua hasimu za Marekani dhidi ya Iran zinakiuka sheria za kimataifa
Aug 20, 2018 09:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuundwa 'jopo kazi la hatua dhidi ya Iran' nchini Marekani ni katika fremu ya sera hasimu za Washington na kinyume cha sheria za kimataifa.
-
Dakta Kharrazi: Vitendo vya kibabe vya Marekani vimesababisha ukosefu wa usalama Mashariki ya Kati
Jul 11, 2018 03:43Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje wa Iran amesema kuwa, uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya nchi nyingine na miamala ya kibabe ya Marekani na utawala haramu wa Israel kuhusiana na Wapalestina ni mambo muhimu ambayo yamechangia mno kukosekana amani na uthabiti katika eneo la magharibi mwa Asia (Mashariki ya Kati)
-
Panetta: Trump anaelekea kuiangamiza Ulaya
Jul 08, 2018 23:56Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kusema kuwa siasa zisizotabirika za Trump zinakaribia kuiangamiza Ulaya.
-
UN: Wahajiri 1,400 wamekufa maji tangu Januari mwaka huu
Jul 06, 2018 22:57Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema zaidi ya wahajiri 1,400 wamefariki dunia katika Bahari ya Mediterania tangu ulipoanza mwaka huu wa 2018 hadi sasa.