Panetta: Trump anaelekea kuiangamiza Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46651-panetta_trump_anaelekea_kuiangamiza_ulaya
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kusema kuwa siasa zisizotabirika za Trump zinakaribia kuiangamiza Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2018 23:56 UTC
  • Panetta: Trump anaelekea kuiangamiza Ulaya

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kusema kuwa siasa zisizotabirika za Trump zinakaribia kuiangamiza Ulaya.

Leon Panetta amesema kuwa viongozi wa nchi za Ulaya wana wasiwasi kwamba Donald Trump anatanguliza mbele sera ya America First (Marekani Kwanza) kuliko muungano wa Transatlantic baina ya Ulaya na Marekani. 

Panetta ameongeza kuwa, watu wa Ulaya wana wasiwasi wa kungamizwa kutokana na siasa zisizoweza kutabirika za Rais wa Marekani, Donald Trump.

Ripoti zinsema kuwa, tishio la kuwaondoa askari wa Marekani barani Ulaya iwapo wanachama wa shirika la kijeshi la NATO hawatalipa gharama za uanachama wao kwa mujibu wa matakwa ya Trump, limezusha wasiwasi mkubwa barani Ulaya.

Donald Trump

Vilevile hatua za Trump za kujiondoa katika mikataba na makubaliano ya kimataifa na kuzidisha ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani kutoka Ulaya vimezidisha wasiwai kuhusu siasa na sera za kiongozi huyo.

Hivi karibuni pia vyombo vya habari duniani viliripoti kwamba, Donald Trump amemshauri Rais Emanuel Macron wa Ufaransa aiondoe nchi yake katika Umoja wa Ulaya.