Indhari kuhusu safari za wahajiri kuelekea Ulaya zenye kuhatarisha maisha
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47873-indhari_kuhusu_safari_za_wahajiri_kuelekea_ulaya_zenye_kuhatarisha_maisha
Mjumbe Maalumu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa katika kituo cha Mediterania ametahadharisha kuwa wahajiri hukabiliana na hatari chungu nzima wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kufika Ulaya.
(last modified 2025-11-19T08:00:07+00:00 )
Sep 03, 2018 13:31 UTC
  • Indhari  kuhusu safari za wahajiri kuelekea Ulaya zenye kuhatarisha maisha

Mjumbe Maalumu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa katika kituo cha Mediterania ametahadharisha kuwa wahajiri hukabiliana na hatari chungu nzima wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kufika Ulaya.

Vincent Kochetel amesema kuwa mtu mmoja kati ya kila wahajiri 18 hupoteza maisha wakati akijaribu kuvuka bahari hiyo ili kuingia Ulaya. Kochetel amebainisha kuwa sababu zinazopelekea kuongezeka hatari katika safari za wahajiri hao ni hatua zinazotekelezwa na magenge ya biashara  haramu ya binamu, za kukabiliana na udhibiti mkali wa doria zinazofanywa na polisi katika pwani ya Libya. 

Wahajiri waliokwama katika bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya

Afisa huyo wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa nchi za Ulaya zinapasa kuchukua hatua za lazima za kuwaokoa wahajiri na kutahadharisha kuwa nchi hizo zinapasa kuziandalia mazingira ya kuingia barani Ulaya familia za watu ambao wanapokelewa kama wakimbizi barani humo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa karibu watu eldu mbili waliaga dunia katika bahari ya Mediterania katika kipindi cha miezi minane ya mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018.