Qassemi: Hatua hasimu za Marekani dhidi ya Iran zinakiuka sheria za kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47568-qassemi_hatua_hasimu_za_marekani_dhidi_ya_iran_zinakiuka_sheria_za_kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuundwa 'jopo kazi la hatua dhidi ya Iran' nchini Marekani ni katika fremu ya sera hasimu za Washington na kinyume cha sheria za kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 20, 2018 09:24 UTC
  • Qassemi: Hatua hasimu za Marekani dhidi ya Iran zinakiuka sheria za kimataifa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuundwa 'jopo kazi la hatua dhidi ya Iran' nchini Marekani ni katika fremu ya sera hasimu za Washington na kinyume cha sheria za kimataifa.

Katika mkutano na waandishi habari mjini Tehran amesema kuundwa 'jopo kazi la hatua dhidi ya Iran' katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na kusema hatua hiyo inakiuka sheria zote zinazojulikana kimataifa. Aidha amesema hatua hiyo haitakuwa na faida yoyote kwa watawala wa Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria jitihada za nchi za Ulaya za kuipa Iran kifurushi cha kiuchumi na pia kuwepo mashirika ya Ulaya nchini na kusema: "Mtazamo wa kisiasa wa Umoja wa Ulaya uko wazi na kumepatikana mafanikio katika kifurishi hicho cha kiuchumi."

Qassemi akijibu swali la mwandishi wa Radio Tehran kuhusu matamshi ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambayo amesema nchi yake inataka kulinda mapatano ya nyuklia ya Iran lakini wakati huo huo ina wasiwasi kuhusu mpango wa makombora ya Iran amesema: "Merkel mwenyewe amesema na hata nchi zilizokuwa katika mazungumzo na Iran katika mapatano ya nyuklia zimeafiki kuwa kadhia ya nyuklia ni tofauti na kadhia ya makombora."