-
UNESCO yaafiki ombi la Rwanda kuhusu kumbukizi za mauaji ya kimbari 1994
May 11, 2017 10:26Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ametangaza kuunga mkono ombi la Rwanda la kutaka maeneo manne yenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yajumuishwe katika orodha ya Turathi za Dunia ya shirika hilo.
-
Makumi ya Wasudan watangaza himaya yao kwa mateka wa Palestina
May 11, 2017 02:52Makumi ya wananchi wa Sudan wameandamana na kukusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa mateka wa Kipalestina.
-
UN: Watoto milioni 2 wa Sudan Kusiniwamelazimika kuwa wakimbizi
May 08, 2017 03:18Umoja wa Mataifa umesema watoto zaidi ya milioni 2 wa Sudan Kusini wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano na ukame vinavyoisakama nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
-
António Guterres aitaka Boko Haram ikomeshe ukiukaji wa haki za watoto
May 05, 2017 09:16Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria kuhitimisha ukiukaji wake wa haki za watoto.
-
UN, US na EU zatakiwa kukomesha jinai za Bahrain dhidi ya Sheikh Qassim
May 05, 2017 09:12Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Bahrain na kimataifa yameziandikia barua Marekani, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya yakizitaka ziishinikize serikali ya Manama kukomesha jinai zake dhidi ya Sheikh Issa Qassim, mwanazuoni mashuhuri wa ngazi ya juu wa nchi hiyo ambaye alivuliwa uraia wa Bahrain Juni 20 mwaka jana 2016.
-
Umoja wa Mataifa waonyesha wasiwasi wake kutokana na kuendelea machafuko Sudan Kusini
May 05, 2017 09:09Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameonyesha wasiwasi mkubwa alionao kutokana na kuendelea mgogoro wa Sudan Kusini na ametoa wito wa kusimamishwa mapigano katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
-
Khoshrou: Matamshi ya Muhammad bin Salman, ni kitisho dhidi ya Iran na kukiri Saudia kuwa inahusika na ugaidi
May 05, 2017 00:08Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa, amesema kuwa matamshi ya hivi karibuni ya Kaimu Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa utawala wa kifalme wa Saudia, ni tishio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na ni kukiri kuwepo ushirikiano wa utawala wa Saudia na vitendo vya ukatili na ugaidi ndani ya Iran.
-
Umoja wa Mataifa waitaka serikali ya Ethiopia kuwaachilia huru wapinzani
May 04, 2017 23:34Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Ethiopia kuwaachilia huru watu ambao walitiwa nguvuni katika maandamano dhidi ya serikali hiyo kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu.
-
Arab League yaitaka UN kufanya uchunguzi juu ya ukatili wanaofanyiwa wafungwa wa Kipalestina katika jela za Israel
May 04, 2017 23:31Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na ukandamizaji wanaofanyiwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
UN yatoa wito wa kuheshimiwa uhuru wa vyombo vya habari
May 03, 2017 02:40Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuenziwa waandishi wa habari na kuheshimiwa uhuru wa vyombo vya habari.