-
Israel yafichua usaliti mpya wa Mahmoud Abbas kwa Wapalestina
Feb 18, 2016 11:36Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amefichua kuwa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alizuia mafuta ya Qatar kufikishwa katika eneo la Ukanda ili kutatua tatizo la fueli katika eneo hilo.
-
Israel yaiomba Ujerumaini iisaidie kuzungumza na HAMAS kuhusu kubadilishana mateka
Feb 17, 2016 11:41Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ameiomba Ujerumani iinasihi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ikubali kubadilishana mateka wa Kipalestina kwa viwiliwili vya wanajeshi wawili wa utawala wa Kizayuni vilivyoko mikononi mwa Hamas.
-
HAMAS: Iran ndiye muungaji mkono wa kweli wa muqawama na taifa la Palestina
Feb 13, 2016 04:42Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, hakuna nchi yoyote ya Kiarabu au ya Kiislamu ambayo hadi hivi sasa imeweza kuifikia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono muqawama na taifa linalodhulumiwa la Palestina.
-
Sheikh Naeem Qassim: Hizbullah haijaghafilika katu na Israel
Feb 12, 2016 23:52Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya muqawa wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, amesema muqawama katu haujaghafilika na njama na vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Umoja wa Mataifa: Utawala wa Kizayuni wa Israel ni mkiukaji wa haki za binadamu
Feb 11, 2016 22:32Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu huko Palestina amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni mkiukaji wa haki za binadamu.
-
Ufuska waongezeka katika familia za kidini za Wazayuni
Feb 10, 2016 11:54Duru za Kizayuni zimeripoti kuwa ufisadi wa kimaadili na ufuska umeongezeka miongoni mwa Waisraeli walioshika dini.
-
Ismail Hania akosoa vikali uungaji mkono usio na mpaka wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni
Feb 04, 2016 12:01Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Marekani ndio mshajiishaji mkuu wa Wazayuni katika uvamizi wao dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Israel kumpa chakula kwa nguvu mfungwa wa Kipalestina
Feb 03, 2016 23:58Utawala haramu wa Kizayuni umepasisha mpango wa kumpa chakula kwa nguvu mwandishi wa habari raia wa Palestina ambaye anashikiliwa katika jela za utawala huo.
-
Ban ailaani tena Israel kwa kughusubu ardhi za Palestina
Feb 02, 2016 00:16Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa mara nyingine ameulaani utawala wa Israel kwa hatua yake ya kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina na kujenga vitongoji vya Wazayuni kinyume cha sheria katika ardhi hizo zilizoghuhusubiwa.
-
HAMAS yapinga mpango wa mapatano wa Ufaransa
Jan 31, 2016 04:02Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema harakati hiyo inapinga mpango wa Ufaransa wa kutaka kuitisha mkutano wa kimataifa kwa lengo kuanzisha tena mazungumzo ya mapatano kati ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.