Ufuska waongezeka katika familia za kidini za Wazayuni
Duru za Kizayuni zimeripoti kuwa ufisadi wa kimaadili na ufuska umeongezeka miongoni mwa Waisraeli walioshika dini.
Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth, limeripoti kuwa wimbi la ufuska na ufisadi wa kiakhlaqi ndani ya jamii ya Wazayuni linazidi kusambaa siku hadi siku na kwamba hivi sasa kumezuka mtindo mpya unaoitwa "kubadilishana wake" ambao umeenea baina ya Mayahudi walioshika dini katika mji wa Haifa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti hilo, mara moja kila baada ya wiki kadhaa, Wazayuni walioshika dini hufanya hafla maalumu katika jengo kubwa ya kubadilishana wake zao.
Viongozi wa utawala wa Kizayuni wamesema wanatiwa wasiwasi na ongezeko la ufisadi wa kimaadili na kifedha ndani ya jamii na katika taasisi za utawala huo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo viongozi kadhaa waandamizi wa utawala wa Kizayuni akiwemo aliyekuwa Rais wa utawala huo Moshe Katsav, mawaziri wa zamani wa mambo ya nje Tzipi Livni na Avigdor Lieberman pamoja na aliyewahi kuwa naibu waziri wa afya Shlomo Benizri wametuhumiwa kuhusika na ufisadi wa kifedha na kiakhlaqi.../