HAMAS yapinga mpango wa mapatano wa Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i301-hamas_yapinga_mpango_wa_mapatano_wa_ufaransa
Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema harakati hiyo inapinga mpango wa Ufaransa wa kutaka kuitisha mkutano wa kimataifa kwa lengo kuanzisha tena mazungumzo ya mapatano kati ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2016 04:02 UTC
  • Hamas senior official
    Hamas senior official

Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema harakati hiyo inapinga mpango wa Ufaransa wa kutaka kuitisha mkutano wa kimataifa kwa lengo kuanzisha tena mazungumzo ya mapatano kati ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ismail Ridhwan, amesema mpango huo haukubaliki na kwamba lengo lake ni kukariri tena njia za hapo kabla zilizogonga mwamba na kufunika jinai za Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.

Msimamo huo wa Hamas wa kupinga mpango wa serikali ya Paris umetangazwa huku Saeb Uraikat, Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema, misimamo iliyoonyeshwa hivi karibuni na Ufaransa ni ishara ya mafanikio ya juhudi za Palestina katika kupigania haki zake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Lauren Fabius alitangaza siku ya Ijumaa kuwa nchi yake inataka kuitisha mkutano wa kimataifa mnamo wiki kadhaa zijazo utakaohudhuriwa na Marekani pamoja na nchi za Ulaya na za Kiarabu kwa lengo la kuanzisha tena mazungumzo ya mapatano baina ya pande mbili za Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.../