Israel yafichua usaliti mpya wa Mahmoud Abbas kwa Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1480-israel_yafichua_usaliti_mpya_wa_mahmoud_abbas_kwa_wapalestina
Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amefichua kuwa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alizuia mafuta ya Qatar kufikishwa katika eneo la Ukanda ili kutatua tatizo la fueli katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 18, 2016 11:36 UTC
  • Israel yafichua usaliti mpya wa Mahmoud Abbas kwa Wapalestina

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amefichua kuwa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alizuia mafuta ya Qatar kufikishwa katika eneo la Ukanda ili kutatua tatizo la fueli katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Kizayuni la Maariv, Moshe Ya'alon, Waziri wa Vita wa utawala huo amefichua kuwa Mahmoud Abbas alipinga pendekezo la kusafirishwa mafuta kutoka Qatar kuelekea Ukanda wa Gaza kupitia bandari ya Israel ya Asdud. Huku akiashiria kuwa asilimia 80 ya kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kuizuia Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) isiwe na satua katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, Ya'alon amesema, ili mamlaka hiyo iweze kuendelea kubaki haiwezi kuvunja ushirikiano wake wa kiusalama na utawala wa Kizayuni.

Utendaji wa karibuni wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina umeonyesha kuwa mamlaka hiyo inayoongozwa na Mahmoud Abbas inafanya kila njia ili kuusambaratisha muqawama katika eneo la Ukanda wa Gaza na vilevile kutekeleza mpango wa Marekani ili kufanikisha sehemu moja ya mkakati mpya wa Washington katika eneo la Mashariki ya Kati kupitia mpango wa "vita dhidi ya ugaidi".../