-
Malengo ya safari ya ghafla ya Saad Hariri nchini Uturuki
Jan 10, 2021 05:46Saad Hariri, waziri mkuu mteule wa Lebanon ambaye amepewa jukumu la kuunda serikali, siku ya Ijumaa alifanya safari ya ghafla na ambayo haikuwa imetangazwa kabla kuelekea nchini Uturuki ambako alikutana na kufanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdoğan.
-
Erdogan: Uturuki inataka kuwa na uhusiano mzuri zaidi na Israel
Dec 25, 2020 23:12Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema nchi yake ingependa iwe na uhusiano mzuri zaidi na Israel na kwamba mazungumzo yanaendelea baina ya pande mbili katika ngazi ya intelijensia.
-
Uturuki yamteua balozi mpya wa Israel baada ya miaka 2
Dec 14, 2020 08:48Uturuki imemteua balozi wake mpya wa Tel Aviv, zaidi ya miaka miwili baada ya Ankara kumuita nyumbani balozi wake aliyekuweko katika utawala haramu wa Israel.
-
Uturuki yakosoa mpango wa nchi za Kiarabu wa kufungua balozi zao Baitul Muqaddas
Nov 28, 2020 04:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema mpango wa nchi za Kiarabu wa kufungua balozi zao katika mji wa Baitul Muqaddas, utadhoofisha uwezekano wa kuundwa nchi ya Palestina.
-
Ghalibaf: Vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi huru, ni siasa zilizofeli
Nov 23, 2020 22:54Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi huru duniani ni siasa zilizofeli na kuongeza kuwa, vikwazo hivyo vimeimarisha misingi ya uchumi wa kutengemea uwezo wa ndani, nchini Iran.
-
Mambo yasiyo na uwazi katika mpango wa amani wa Russia kuhusu mgogoro wa Karabakh
Nov 16, 2020 06:49Mambo ya kutiliwa shaka na yasiyofahamika vizuri katika mkataba wa amani wa Russia kuhusu mgogoro wa Azerbaijan na Armenia juu ya eneo la Nagorno Karabakh, yamenyamaziwa kimya na viongozi wa Azerbaijan na Uturuki.
-
Baada ya kuzingirwa kila upande, wanajeshi wa Uturuki waondoka kwenye kambi nyingine nchini Syria
Nov 08, 2020 07:58Duru mbalimbali za habari zimetangaza kuwa, wanajeshi wa Uturuki wameondoka katika kambi nyingine ya viunga vya kusini mwa mji wa Idlib wa magharibi mwa Syria na kukimbilia katika maeneo mengine yanayodhibitiwa na waasi wa nchi hiyo.
-
Onyo la Lavrov kuhusu uwepo wa mamluki 2000 wa kitakfiri huko Karabakh
Nov 05, 2020 00:28Russia daima imekuwa ikitahadharisha kuhusu hatari ya uwepo wa makundi ya kigaidi yenye misimamo ya kupindukia mpaka katika nchi hiyo na nchi nyingine za Caucasia na Asia ya Kati na kusisitiza udharura wa kupambana na makundi hayo.
-
Erdogan: Dunia ipige vita uadui dhidi ya Uislamu sawa ilivyo katika suala la kupiga vita Uyahudi
Nov 02, 2020 23:15Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ameitaka dunia ijifunze na kupata somo na ibra kutokana na uzembe wa jamii ya kimataifa iliyoacha kuzuia mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Bosnia Herzegovina na kusisitiza kuwa, dunia inapaswa kupiga marufuku na kupambana na chuki na uhasama dhidi ya Uislamu kama ilivyopambana na chuki dhidi ya Uyahudi baada ya Holocaust (yanayodaiwa kuwa mauaji ya Mayahudi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia).
-
Waliouawa katika zilzala ya Izmir, Uturuki wapindukia 50
Nov 02, 2020 00:59Idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mjini Izmir nchini Uturuki imeripotiwa kufika 51, huku timu za uokoaji zikiendelea kutafuta manusura na maiti zilizokwama chini ya vifusi vya nyumba na majengo yaliyobomolewa na zilzala hiyo.