Lebanon yazishutumu Uturuki na Israel kuifanyia utapeli
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65819-lebanon_yazishutumu_uturuki_na_israel_kuifanyia_utapeli
Wizara ya Viwanda ya Libanon imezishutumu Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuitapeli na kuwadanganya watumiaji wa bidhaa za madola hayo katika masoko ya kigeni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 17, 2021 09:51 UTC
  • Lebanon yazishutumu Uturuki na Israel kuifanyia utapeli

Wizara ya Viwanda ya Libanon imezishutumu Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuitapeli na kuwadanganya watumiaji wa bidhaa za madola hayo katika masoko ya kigeni.

Shirika la habari la ISNA limeripoti habari hiyo leo na kunukuu taarifa ya Wizara ya Viwanda ya Lebanon ikilalamikia vikali utapeli hiyo na kusisitiza kwamba, ina taarifa za uhakika na picha zinazoonesha jinsi Uturuki na utawala wa Kizayuni zinavyotumia logo na nembo za Lebanon kwenye bidhaa zao za chakula ili kuonesha kuwa ni za Lebanon.

Katika taarifa yake hiyo, Wizara ya Viwanda ya Lebanon imesema, kitendo hicho cha Uturuki na utawala wa Kizayuni ni utapeli, ni wizi na ni jinai isiyo na mithili, dhidi ya haki ya kujitawala, haki ya kiuchumi na haki ya bidhaa na viwanda ya Lebanon. Aidha imesema itavikabidhi ushahidi wake huo vyombo vya habari vya ndani na nje ya Lebanon na suala hilo litafuatiliwa pia kidiplomasia na vyombo vya Lebanon vilivyoko nje ya nchi.

 

Katika miezi ya hivi karibuni Lebanon imekumbwa na migogoro mbalimbali kutokana na matatizo ya kifedha, kiuchumi na maandamano makubwa ya wananchi ya kulalamikia utendaji wa taasisi za serikali. Ombwe la kutokuweko serikali nchini Lebanon ni mgogoro mwingine mkubwa nchini humo.

Kusambaratika viwanda ya Lebanon kumezorotesha mno uchumi wa taifa na nafasi za ajira pamoja na mchakato wa uzalishaji bidhaa nchini humo na suala hilo linachangiwa na madola kama utawala wa Kizayuni na Uturuki ambayo yanamimina bidhaa zao masokoni kwa jina la Lebanon.