Baada ya kuzingirwa kila upande, wanajeshi wa Uturuki waondoka kwenye kambi nyingine nchini Syria
(last modified Sun, 08 Nov 2020 11:28:36 GMT )
Nov 08, 2020 11:28 UTC
  • Baada ya kuzingirwa kila upande, wanajeshi wa Uturuki waondoka kwenye kambi nyingine nchini Syria

Duru mbalimbali za habari zimetangaza kuwa, wanajeshi wa Uturuki wameondoka katika kambi nyingine ya viunga vya kusini mwa mji wa Idlib wa magharibi mwa Syria na kukimbilia katika maeneo mengine yanayodhibitiwa na waasi wa nchi hiyo.

Shirika la habari la ISNA ni miongoni mwa mashirika yaliyoripoti habari hiyo leo na kuongeza kuwa, zaidi ya malori 50 yenye zana za kila namna za kijeshi ya Uturuki yameondoka katika kambi nyingine ya kijeshi ya mji wa Ma`arat al-Nu`man kwenye viunga vya kusini mwa mkoa wa Idlib na kukimbilia katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi ya Jabal al Zawiya.

Katika siku zilizopita pia duru za Syria zilitangaza habari ya kukimbia wanajeshi vamizi wa Uturuki katika kambi nne za kijeshi kwenye mikoa ya Hama na Idlib.

Jeshi la Syria

 

Wanajeshi wa Syria wanalazimika kuondoka katika kambi za kijeshi ndani ya ardhi ya Syria kutokana na wanajeshi wa nchi hiyo ya Kiarabu kuzizingira kambi hizo za kijeshi za wanajeshi vamizi wa Uturuki. Tangu mwezi Januari hadi hivi sasa, wanajeshi wa Syria wamekuwa wakikomboa maeneo zaidi yaliyovamiwa na madola ya kigeni. Wavamizi hao wameingia Syria kiuvamizi kwa madai ya kupambana na ugaidi. Wanajeshi na wananchi wa Syria wamefanikiwa kuwalazimisha wavamizi hao na vibaraka wao kukimbia kwenye maeneo mengi waliyoyavamia.

Uturuki imetuma wanajeshi wake nchini Syria kwa kisingizio cha kupambana na waasi wa Kikurdi wa PKK na kwa muda mrefu inayakalia kwa mabavu maeneo ya kaskazini mwa Syria.

Serikali ya Syria inasema kuwa, uvamizi huo wa Uturuki na madola mengine ya kigeni unakanyaga sheria zote za kimataifa, ni kuktoheshimu uhuru wa kujitawala taifa la Syria hivyo lazima wavamizi wote waondoke katika kila shibri ya ardhi ya Syria.

Tags