Maandamano makubwa ya wananchi wa Jordan na Uturuki kulaani jinai za Israel Gaza
(last modified Fri, 18 Oct 2024 07:53:05 GMT )
Oct 18, 2024 07:53 UTC
  • Maandamano makubwa ya wananchi wa Jordan na Uturuki kulaani jinai za Israel Gaza

Maelfu ya wananchi wa Jordan na Uturuki wameandamana na kulaani jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano hayo yamefanyika baada ya kutangazwa habari isiyo rasmi ya kuuawa shahidi Yahya al-Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Waandamanaji nchini Jordan wamekusanyika mbele ya ubalozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kupiga nara za kulaani jinai za wazayuni dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamelaani jinai za Israel na kutoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kusitisha jinai hizo za Israel.

Maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia nchini Uturuki ambako kama ilivyokuwa Jordan nao wamepaza sauti kulaani jinai za Israel.

Jana vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vilitangaza kuwa, vimemuua Yahya al-Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, habari ambayo hadii sasa bado haijathibitishwa na harakati ya HAMAS.

Tags