Uturuki yajiunga rasmi na kesi ya Afrika Kusini ICJ dhidi ya Israel
(last modified Sat, 10 Aug 2024 02:33:29 GMT )
Aug 10, 2024 02:33 UTC
  • Uturuki yajiunga rasmi na kesi ya Afrika Kusini ICJ dhidi ya Israel

Uturuki imetangaza kuwa, imewasilisha rasmi ombi la kujiunga na kesi ya Afrika Kusini iliyowasilishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ).

Mkuu wa Kamati ya Kisheria ya Bunge la Utuuruki amesema kuwa, kuna Ushahidi mwingi unaoonyesha kuwa utawala ghasibu wa Israel umetenda jinai na mauaji ya kimbari katika ukanda wa Gaza.

Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ imethibitisha kuwasilishwa kwa ombi la Uturuki la kujiunga na Afrika Kusini katika kesi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel, ICJ, mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa, ilitoa hatua tatu za muda Januari 26, Machi 28 na Mei 24.

Majaji wa Afrika Kusini wakiwa katika ukumbi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ)

 

ICJ iliiamuru Israel kuchukua hatua zote ndani ya uwezo wake kuzuia mauaji ya kimbari huko Gaza, kuruhusu upatikanaji wa chakula bila vikwazo katika eneo la Palestina lililozingirwa, na kusitisha mara moja uvamizi wake wa kijeshi katika mji wa kusini wa Rafah. Israel imepuuza maagizo hayo yote ya ICJ.

Sasa  Uturuki inaungana rasmi na mataifa mengine mengi kama Cuba, Nicaragua, Colombia, Libya, Maldives, Misri, Ireland, Ubelgiji, Uturuki, Chile na kadhalika ambayo yametangaza kujiunga na shtaka la Afrika Kusini dhidi ya Israel katika mahakama ya ICJ.   

Tags