Shambulio la kinyama la Israel katikati ya Beirut laua Walebanon 22 na kuwajeruhi wengine 117
(last modified Fri, 11 Oct 2024 07:44:48 GMT )
Oct 11, 2024 07:44 UTC
  • Shambulio la kinyama la Israel katikati ya Beirut laua Walebanon 22 na kuwajeruhi wengine 117

Utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya shambulizi la kinyama la anga katikati mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut nje ya viunga vya kusini mwa mji huo, na kuua watu wasiopungua 22 na kujeruhi wengine wengi.

Wizara ya Afya ya Umma ya Lebanon imetangaza kuwa watu wasiopungua 22 waliuawa shahidi na wengine 117 walijeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel mjini Beirut jana jioni ambayo yalibomoa majengo mawili ya makazi ya raia.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, idadi kubwa ya watu walijeruhiwa na kupelekwa hospitali zilizoko karibu na viunga jirani.
 
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, watu walionekana wakiwa wamejawa na huzuni na majonzi nje ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Beirut Medical Center, ambapo baadhi ya majeruhi walikuwa wakipatiwa matibabu.
Eneo lililoshambuliwa

Watu waliokuwapo nje ya hospitali waliwaambia waandishi wa habari kwamba waliona michirizi angani na, bila shaka, miripuko mikubwa.

Wakati wa shambulio hilo la kinyama la Israel lililolenga katikati ya mji mkuu wa Lebanon, watu walikuwa wakikimbia na kupiga makelele katika viunga vya mji huo, wakiwa wamepatwa na kiwewe kikubwa.
 
Walebanon wengi wametoka viunga vya kusini mwa Beirut na wamepata hifadhi katika viunga vilivyofurika watu katikati mwa mji mkuu huo wa Lebanon. Takriban watu 700,000 wamelazimika kuhama makazi yao kutoka viunga hivyo na kukimbilia kwenye maeneo hayo.
 
Wizara ya Afya ya Lebanon imesema, tangu Oktoba 2023 hadi sasa, zaidi ya watu 2,141 wameuawa shahidi na wengine 10,099 wamejeruhiwa katika mashambulio ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, wakiwemo makumi ya watoto na wanawake wengi.../

Tags