-
Waba waua watu 18 nchini Zimbabwe
Sep 11, 2018 10:11Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare ametangaza kuwa mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu na homa ya matumbo umeua watu wasiopungua 18 katika jiji hilo katika wiki moja iliyopita.
-
Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare
Sep 11, 2018 07:13Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amesema watu wasiopungua 16 wamefariki dunia wiki iliyopita kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
-
UN: Msaada wa haraka unahitajika kwa waathirika wa baa la njaa Zimbabwe
Sep 03, 2018 14:11Msemaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) amesema kuwa shirika hilo linahitajia msaada wa haraka wa zaidi ya tani milioni moja za chakula kwa ajili ya raia walioathiriwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
-
Mahakama Zimbabwe yatupilia mbali madai ya wapinzani, yaidhinisha ushindi wa Mnangagwa kama rais
Aug 24, 2018 14:42Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na wapinzani na kumuidhinisha Emmerson Mnangagwa kama rais wa nchi hiyo. Chama kikuu cha upinzani cha MDC kilikuwa kimepinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita wa Julai kwa madai ya kuwepo wizi wa kura.
-
Mbivu mbichi kujulikana leo Zimbabwe kuhusu ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa
Aug 24, 2018 08:20Raia wa Zimbabwe wana shauku kubwa ya kujua hukumu inayotazamiwa kutolewa na Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo kuhusu kesi iliyowasilisha na kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa kupinga ushindi wa Rais Emmersom Mnangagwa katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 mwaka huu.
-
Mbunge wa Uganda Bobi Wine kufikishwa katika mahakama ya kijeshi leo
Aug 23, 2018 04:47Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi kwa jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Mahakama ya Katiba Zimbabwe yaanza kusikiliza kesi kuhusu uchaguzi wa rais
Aug 22, 2018 07:53Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe inaanza kusikiliza leo, kesi ya chama kikuu cha upinzani MDC kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangangwa.
-
Rais Mnangagwa awataka Wazimbabwe kusonga mbele baada ya machafuko ya uchaguzi
Aug 14, 2018 03:17Rais Emmerson Mnangangwa wa Zimbabwe jana alisema kuwa Wazimbabwe wanapaswa kuwa kitu kimoja ili kujenga uchumi wa nchi yao na kuwenda kando kipindi cha uchaguzi. Watu sita waliuawa katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa rais huko Zimbabwe mwezi huu.
-
Hafla ya kuapishwa Rais wa Zimbabwe yaakhirishwa ili kusubiri uamuzi wa kesi ya wapinzani
Aug 11, 2018 14:25Hafla ya kuapishwa Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye alishinda katika uchaguzi wa Julai 30 imeakhirishwa baada ya wapinzani kuwasilisha kesi mahakamani wakipinga matokeo ya uchaguzi huo.
-
Chamisa awasilisha hoja mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi Zimbabwe
Aug 11, 2018 04:03Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa jana Ijumaa aliwasilisha mahakamani hoja ya kupinga ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini humo.