Wanafunzi wanaume Waislamu Uswisi wasameheka kuwapa mkono walimu wao wa Kike
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i4483-wanafunzi_wanaume_waislamu_uswisi_wasameheka_kuwapa_mkono_walimu_wao_wa_kike
Wanafunzi Waislamu wa Manispaa ya Therwil katika jimbo la Basel nchini Uswisi hawatohitajika tena kuwapa mikono walimu wao wa kike kufuatia uamuzi uliotolewa Mamlaka za Elimu katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 05, 2016 11:30 UTC
  • Wanafunzi wanaume Waislamu Uswisi wasameheka kuwapa mkono walimu wao wa Kike

Wanafunzi Waislamu wa Manispaa ya Therwil katika jimbo la Basel nchini Uswisi hawatohitajika tena kuwapa mikono walimu wao wa kike kufuatia uamuzi uliotolewa Mamlaka za Elimu katika eneo hilo.

Maafisa wa elimu wa eneo la Therwil wamefikia uamuzi huo ambao umezusha mjadala na makelele nchini Uswisi baada ya wanafunzi wawili wa kiume Waislamu kualalmika kwamba mila na desturi za Uswisi za kupeana mikono na mwalimu zinakinzana na imani yao ya kidini endapo mwalimu huyo atakuwa ni wa kike. Wanafunzi hao walibainisha katika malalamiko yao kuwa Uislamu hauruhusu mtu kugusana kimwili na mwenzake wa jinsia tofauti isipokuwa watu ambao ni maharimu zake katika familia.

Hata hivyo uamuzi huo ulioptishwa na Mamlaka za Elimu katika eneo hilo umezusha makelele nchini Uswisi. Felix Mueri mkuu wa Kamati ya Bunge ya Sayansi, Elimu na Utamaduni amesisitiza kuwa kupeana mikono ni sehemu ya utamaduni wa nchi hiyo.

Christoph Eymann, ambaye ni mkuu wa Baraza Kuu la Mawaziri wa Elimu wa majimbo yote ya Uswisi amedai kuwa hawawezi kuvumilia wanawake watendewe kinyume na wanaume katika huduma za jamii.

Hata hivyo licha ya malalamiko hayo, uongozi wa jimbo la Basel ambao ndio wenye mamlaka ya kutengua uamuzi huo uliopitishwa na mamlaka za elimu za eneo la Therwil haujatoa tamko lolote juu ya suala hilo hadi sasa.../