Mtangazaji apigwa kibao akiwa LIVE hewani, kulikoni?
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i7519-mtangazaji_apigwa_kibao_akiwa_live_hewani_kulikoni
Mtangazaji wa televisheni ya Russia Today bila ya kutarajia alishitukia anazabwa kibao na mmoja wa waandamanaji wakati alipokuwa LIVE hewani akitoa ripoti kuhusu maandamano mapya ya wafanyakazi jijini Paris, Ufaransa.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 21, 2016 12:44 UTC

Mtangazaji wa televisheni ya Russia Today bila ya kutarajia alishitukia anazabwa kibao na mmoja wa waandamanaji wakati alipokuwa LIVE hewani akitoa ripoti kuhusu maandamano mapya ya wafanyakazi jijini Paris, Ufaransa.

Kipande hiki cha video kinaonesha namna mtangazaji huyo alivyodhibiti nafsi yake akaendelea na ripoti yake licha ya kuendelea kusumbuliwa na waandamanaji.

Ni vyema kusema hapa kwamba, hivi sasa mji mkuu wa Ufaransa, Paris, unashuhudia maandamano makubwa ya wafanyakazi wanaopinga sheria mpya zilizowekwa na Rais Francois Hollande wa nchi hiyo.