Oct 04, 2024 07:59 UTC

Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimesambaza mkanda wa video na ndani yake wanatangaza kuwa operesheni hiyo ni zawadi kwa shahid wa Muqawama, Sayyid Hassan Nasrullah. Mkanda huo unaonesha mtego kabambe waliowawekea wanajeshi katili wa Israel na vifaru na mabuldoza yao na namna vinavyoteketezwa kimoja baada ya kingine huko Khan Yunus, katika Ukanda wa Ghaza.

Ndani ya mkanda huo, makamanda wa HAMAS wanasema, operesheni hii kabambe tumeifanya ikiwa ni zawadi ya taifa la Palestina kwa ndugu zao wa Lebanon, hasa Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah.

Fuatilia video hii hapa chini uone zawadi ya tunu ya HAMAS kwa Sayyid Hassan Nasrullah na namna harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina inavyotoa vipigo na kuwati hasa wanajeshi wa Israel.

Tags