Magaidi wafanya shambulio jingine baya la kigaidi Mali + Video
https://parstoday.ir/sw/news/event-i122486-magaidi_wafanya_shambulio_jingine_baya_la_kigaidi_mali_video
Takriban watu 40 wameuawa baada ya genge la kigaidi la Daesh (ISIS) kushambulia msafara wa usambazaji bidhaa katika nchi ya Kiafrika ya Mali.
(last modified 2025-10-17T12:36:14+00:00 )
Feb 09, 2025 02:24 UTC
  • Magaidi wafanya shambulio jingine baya la kigaidi Mali + Video

Takriban watu 40 wameuawa baada ya genge la kigaidi la Daesh (ISIS) kushambulia msafara wa usambazaji bidhaa katika nchi ya Kiafrika ya Mali.

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Fars na kuongeza kuwa, magaidi wa Daesh (ISIS) barani Afrika, wamechoma moto magari matano katika shambulio dhidi ya msafara wa usambazaji bidhaa nchini Mali.

Msafara huo ulikuwa unaongozwa na jeshi lakini wanajeshi hawakuweza kujilinda mbele ya mashambulizi makali ya magaidi wa ISIS kwani walikuwa wamewekewa mtego na kushambuliwa kwa risasi nyingi na kwa mada za miripuko.

Kabla ya hapo gazeti la Daily Star la Mali lilikuwa limeripoti kutokea shambulio dhidi ya msafara uliokuwa unaongozwa na jeshi la Wagner Group kaskazini mwa Mali. Gazeti hilo lilisema, watu 10 wameuawa kwenye shambulio hilo. 

 

Shambulio hilo limekuja wiki moja baada ya Jeshi la Mali kutangaza kuwa limemuangamiza kiongozi wa genge la kigaidi aliyekuwa anaogoza vitendo vya kigaidi katikati mwa Mali.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, magaidi wengine kadhaa nao waliangamizwa wakati wa operesheni kubwa iliyofanyika kote nchini Mali wiki iliyopita. 

Taarifa ya jeshi la Mali lilitaja jina la kiongozi huyo wa magaidi aliyeangamizwa kuwa Amadou Bolly na alikuwa akiongoza vitendo vya kigaidi katika eneo la Kolongo. Aliuawa kwa kupigwa risasi pamoja na wenzake kadhaa katika operesheni iliyofanyika kwenye maeneo ya Niaro, Nossombougou, Maninie, N'djibala, Boky Were na Kononga katikati mwa Mali.