Syria yasisitiza kuunga mkono kadhia ya Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i100476-syria_yasisitiza_kuunga_mkono_kadhia_ya_palestina
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imesisitiza juu ya misingi na misimamo yake thabiti na isiyoteereka ya kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina ambalo ardhi yake inakabiliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 30, 2023 04:33 UTC
  • Syria yasisitiza kuunga mkono kadhia ya Palestina

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imesisitiza juu ya misingi na misimamo yake thabiti na isiyoteereka ya kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina ambalo ardhi yake inakabiliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imebainisha kwamba, taifa hilo litaendelea kuwa katika orodha ya mataifa yanayoliunga mkono na kulitetea taifa la Palestina.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imesisitiza kwamba, mbali na uungaji mkono wa Damascus kwa Palestina, taifa hilo litaendelea kufanya kila liwezalo kuhakikisha kwamba, ukaliaji mabavu dhidi ya Palestina unafikia kikomo na kwamba, katu haitaacha kufanya juhudi katikak uwanja huo.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria iimesema pia katika taarifa yake hiyo ya kwamba, katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) iimesisitizwa kwamba,  taifa la Palestina linapaswa kuwa na haki ya kujianishia hatima na mustakabali wake na hivyo iweze kuasisi dola la Palestina mjii mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika miiezi ya hivi karibuni utawala ghasibu wa Israel umeshadidisha jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina.

Mwezi uliopita wa Juni, mawakili wa wawakilishi 8 wa Bunge la Palestina wamewasilisha kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya utawala vamizi wa Israel, kutokana na mzingiro wa Ukanda wa Gaza unaoendelea kwa miaka mingi.