UNRWA yatoa indhari: Baa la ukame linakaribia kuumeza Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i100504-unrwa_yatoa_indhari_baa_la_ukame_linakaribia_kuumeza_ukanda_wa_gaza
Mshauri wa vyombo vya habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Wapalestina UNRWA ametahadharisha kuwa baa halisi la njaa linakaribia kuumeza Ukanda wa Gaza katika miezi kadhaa ijayo kutokana na kuendelea kwa hali mbaya ya uhaba wa fedha unaosababishwa na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 30, 2023 23:38 UTC
  • UNRWA yatoa indhari: Baa la ukame linakaribia kuumeza Ukanda wa Gaza

Mshauri wa vyombo vya habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Wapalestina UNRWA ametahadharisha kuwa baa halisi la njaa linakaribia kuumeza Ukanda wa Gaza katika miezi kadhaa ijayo kutokana na kuendelea kwa hali mbaya ya uhaba wa fedha unaosababishwa na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa.

Mnamo Januari 2018, Marekani ilikata msaada wake wa dola milioni 300 kwa shirika la UNRWA kwa lengo ya kuwashinikiza Wapalestina waukubali mpango wa mapatano wa kihaini uliopewa jina la Muamala wa Karne.
Kwa mujibu wa shirika la habari la SAMA, Adnan Abu Husna, mshauri wa vyombo vya habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), amesema, "tunakabiliwa na punguzo la misaada ya kimataifa, ambayo imeathiri si Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP pekee, lakini mashirika yote ya kimataifa."

Abu Husna amesisitiza kuwa UNRWA inatoa msaada wa chakula na pesa taslimu kwa Wapalestina 1,700,000 wa Gaza, Ukingo wa Magharibi na Syria. Shirika hilo hutoa msaada wa chakula kwa mpangilio maalumu kwa wakimbizi 1,200,000 wa Ukanda wa Gaza. Iwapo misaada hiyo itasitishwa, -na uwezekano ni mkubwa-, Gaza itakabiliwa na baa halisi la njaa katika miezi ijayo.

 
Afisa huyo wa UNRWA ameeleza kuwa asilimia 80 ya wakazi wa Gaza wanaishi maisha ya ukimbizi, na kwamba wakimbizi 800,000 hawawezi kujikimu milo miwili kwa siku, na hiyo ni hatari.
 
Abu Husna ameongeza kuwa, "tumeitangazia dunia kwamba tunahitaji kwa haraka dola milioni 70 kununua chakula kwa ajili ya Ukanda wa Gaza, na pia tunahitaji dola milioni 30 ili kusambaza msaada wa fedha taslimu kwa wakimbizi walioko Lebanon na Syria".../