Mejenerali Wazayuni watiwa kiwewe na nguvu za makombora za Wapalestina
Majenerali wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wametiwa kiwewe na nguvu za makombora zinazozidi kuongezeka za wanamapambano wa Palestina hasa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na hususa kwenye mji wa Jenen.
Hayo yameripotiwa na gazeti la Kizayuni la "Israel Hayom" ambalo limewanukuu majenerali watatu wakubwa wa jeshi la Israel wakikiri kwamba uwezo wa makombora wa Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan si kitu cha kudharauliwa.
Mejenerali hao Wazayuni aidha wamesema, mwanzoni mwa mwaka 2000 na kuendelea tulishuhudia harakati kama hizo katika Ukanda wa Ghaza na kila muda ulivyopita ndivyo Wapalestina walivyojiimarisha zaidi kwa nguvu za makonmbora na sasa wamekuwa ni tishio kwa Israel kwani makombora hayo yanazalishwa ndani ya Ukanda wa Ghaza kwenyewe hayaagiziwi kutoka nje.
Kuongezeka nguvu za makombora za Wapalestina pamoja na uwezo wao wa kijeshi katika masuala mengine yakiwemo ya kuzalisha na kufanyia majaribio silaha zao na kuanza kutumia makombora kushambulia vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na taasisi za Wazayuni kutoka Ukingo wa Magharibi, ni katika mambo ambayo yamewatia wasiwasi mkubwa Wazayuni ambao wanaamini kuwa mashambulio kutoka Ukingo wa Magharibi ni hatari zaidi kwao kuliko hata ya Ukanda wa Ghaza.
Gazeti hilo la Kizayuni la "Israel Hayom" vilevile limeandika katika ripoti yake kwamba, katika kipindi cha chini ya miezi mitatu tu iliyopita, Wapalestina wametoa matamko 6 ya kushambulia kwa makombora vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kutokea mji wa Jenin. Matamshi hayo yametolewa chini ya jina la Brigedi za Ayyash.
Ripoti ya gazeti hilo la Kizayuni imeongeza kuwa, chanzo cha kushambuliwa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa kutumia makombora yanayozalishwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan sambamba na operesheni nyingine nyingi za Wapalestina ni jinai za utawala wa Kizayuni katika Msikiti wa al Aqsa.