Haaretz: Mgogoro wa kushindwa jeshi la Israel unazidi kupanuka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i100748-haaretz_mgogoro_wa_kushindwa_jeshi_la_israel_unazidi_kupanuka
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kuwa matatizo yanayowapata wanajeshi wa utawala huo ni makubwa mno kuliko kile kinachoelezwa na maafisa usalama wa Tel Aviv.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 06, 2023 07:17 UTC
  • Haaretz: Mgogoro wa kushindwa jeshi la Israel unazidi kupanuka

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kuwa matatizo yanayowapata wanajeshi wa utawala huo ni makubwa mno kuliko kile kinachoelezwa na maafisa usalama wa Tel Aviv.

Rasimu ya mpango wa marekebisho ya mahakama uliopendekezwa na baraza la mawaziri la Netanyahu mwezi Januari mwaka huu limesababisha ufa mkubwa kati ya viongozi wa Israel na kuibua maandamano makubwa ya upinzani ndani ya utawala wa Kizayuni.  

Maandamano ya mitaani na malalamiko ya kisheria ya muungano wa upinzani katika bunge la Knesset dhidi ya baraza la mawaziri la Netanyahu yameshadidi baada ya kupasishwa kipengee kilichoibua utata na makelele mengi cha marekebisho hayo. 

Benjamin Netanyahu 

Vyombo vya habari vya Israel leo vimeripoti kuwa, utendaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni umepungua kwa kuzingatia maandamano ya askari wa akiba wa utawala huo wanaopinga mpango huo wa kubadili sheria za mahakama za Israel. 

Amos Harel, mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa gazeti la Haaretz anasema: Utendaji wa jeshi la Israel umeporomoka katika nyuga zote kutokana na maandamano makubwa ya kupinga mageuzi hayo, na kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo mzozo unavyozidi kuwa mkubwa.