Jumuiya ya Wanahabari: Mashia wanaendelezwa kukandamizwa nchini Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i100764-jumuiya_ya_wanahabari_mashia_wanaendelezwa_kukandamizwa_nchini_bahrain
Jumuiya ya Wanahabari wa Bahrain imetangaza kuwa,utawala wa Al-Khalifa unaendelea kuwatesa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 06, 2023 23:12 UTC
  • Jumuiya ya Wanahabari: Mashia wanaendelezwa kukandamizwa nchini Bahrain

Jumuiya ya Wanahabari wa Bahrain imetangaza kuwa,utawala wa Al-Khalifa unaendelea kuwatesa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Taarifa ya jumuiya hiyo mbali na kulaani hatua za mateso na ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Bahrain imeutaka utawala huo wa kifamilia kukomesha vitendo hivyo.

Jumuiya ya Wanahabari wa Bahrain imetangaza kuwa tangu mwaka 2011, utawala wa Al-Khalifa haujaacha kutumia visingizio bandia kuwatesa raia wake wa Kishia na umeweka vikwazo vya kufanya maombolezo katika mwezi wa Muharram hatua ambazo zinakinzana na uhuru wa kidini.

Kulingana na ripoti hii, vyombo vya usalama ya utawala wa Al Khalifa vimewatia mbaroni makumi ya Waislamu wa Kishia kwa kile kilichoelezwa kuwa, kuzuia ukusanyaji wa nembo na alama za kkumbuukumbu ya Ashura. Vikosi vya usalama vilikuwa vikizitaka familia hizo kukabidhi alama na mabango ya Ashura, huku familia hizo zikiandamwa kwa vitisho vya simu na wakati mwingine kuitwa katika vituo vya polisi.

 

Wakati huo huo, Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain kimetangaza kuwa, zaidi ya matukio 100 ya ukiukaji wa haki za binadamu yameripotiwa nchini humo katika kipindi cha mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo hicho cha haki za binadamu, wananchi wa maeneo mbalimbali ya Bahrain wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja pekee zaidi ya matukio 100 ya ukiukaji wa haki za binadamu yameripotiwa nchini humo.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha, ubaguzi wa kidini na kimadhehebu na kubomolewa misikiti ya Waislamu wa Kishia ni miongoni mwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyoshuhudiwa nchini Bahrain.