Sep 10, 2023 07:30 UTC
  • Magaidi zaidi ya 100 waangamizwa katika mji wa Idlib Syria

Zaidi ya magaidi 100 wameangamizwa nchini Syria na kutoa pigo kwa mabaki ya wapiganaji wa kigaidi katika nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Syria imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo likishirikiana ana vikosi vya Russia limefanikiwa kuangamiza zaidi ya magaidi 100 katika mji wa Idlib.

Kundi la kigaidi la Tahrir al-Sham (Jabhat Al-Nusra), ambalo daima limekuwa likishindwa mtawalia na jeshi la Syria na vikosi vya muqawama wa Kiislamu katika maeneo tofauti ya nchi hii, bado lipo katika baadhi ya maeneo nchini Syria kwa uungaji mkono wa Uturuki na inaendelea na vitendo vyake vya uhasamana harakati za kigaidi.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, kundi la kigaidi la Daesh au jina jingine ISIS, limezidisha mashambulizi yake katika ardhi ya Syria.

Shirika la habari la Associated Press limesema katika ripoti kwamba kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limesema katika ripoti kwa Baraza la umoja huo kwamba katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, tishio la Daesh limeongezeka katika baadhi ya maeneo yenye migogoro huko Iraq na Syria. Kwa mujibu wa shirika hilo la habari, ripoti ya wataalamu hao inasema licha ya Daesh kupata hasara na maafa makubwa katika shughuli zake katika nchi za Syria na Iraq na kupungua operesheni zake za kigaidi katika nchi hizo, lakini bado kuna hatari ya kuimarika tena.

Mbali na kuendelea kuiweka Syria katika hali ya ghasia na udhaifu, Marekani pia inafuatilia njama za kuziwekea mashinikizo nchi za Iran na Russia nchini Syria kupitia juhudi za kuwarejesha magaidi wa Daesh katika ardhi ya Syria.

Tags