Mkuu wa Jumuiya wa kuihami Palestina: Watu wa Gaza watashinda
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104112-mkuu_wa_jumuiya_wa_kuihami_palestina_watu_wa_gaza_watashinda
Mkuu wa Jumuiya ya Kuihami Palestina ameeleza kuwa watu wa Gaza wamesimama imara na kwa nguvu zote katika kupigania haki yao na kusisitiza kuwa kwa hakika watu wa Gaza watashinda na hakuna shaka katika hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 30, 2023 03:29 UTC
  • Mkuu wa Jumuiya wa kuihami Palestina: Watu wa Gaza watashinda

Mkuu wa Jumuiya ya Kuihami Palestina ameeleza kuwa watu wa Gaza wamesimama imara na kwa nguvu zote katika kupigania haki yao na kusisitiza kuwa kwa hakika watu wa Gaza watashinda na hakuna shaka katika hilo.

Wanamuqawama wa Palestina tarehe 7 mwezi huu walianzisha oparesheni ya kushtukiza kwa jina la "Kimbunga cha Al Aqsa" kutokea Gaza kusini mwa Palestina dhidi ya ngome za utawala unaokalia Quds kwa mabavu ili kujibu jinai za utawala haramu wa Kizayuni; na utawala huo sasa umefunga vivuko vyote vya Gaza na unaendelea kushambulia kwa mabomu maeneo ya raia na vituo vya matibabu katika eneo hilo ili kulipiza kisasi, kufidia kushindwa kwake na kusitisha oparesheni ya wanamuqawama wa Palestina.  

Shirika la habari la IRNA limearifu kuwa, Hujjatul Islam Muhammad Hassan Rahimian Mkuu wa Jumuiya ya Kuihami Palestina ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni kila dakika unawaua watu wa Gaza kwa kutumia ndege 150 za kivita pamoja na silaha dhidi ya binadamu.   

Mashambulio ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza

Hujjatul Islam Rahimian ameongeza kuwa, raia wa Ukanda wa Gaza licha ya mazingira haya magumu lakini wako imara na wanapambana ili kutetea haki zao, na kwa hakika raia hao wataibuka na ushindi na hakuna shaka yoyote katika hilo. 

Mkuu wa Jumuiya ya Kuihami Palestina ameashiria kushindwa Israel kuanzia vita vya siku 33 hadi katika Kimbunga cha Al Aqsa na kusema uongo wa madai ya kutoshindwa Israel vitani umethibitishwa wazi mara kadhaa na kuongeza kuwa: Mwenendo wa sasa unawaonyesha wapigania uhuru mustakbali wao ulio wazi ambao utakuwa ni kufutiliwa mbali Israel katika uso wa dunia, na zaidi ya hapo ni kuangamizwa Marekani, ambapo dalili za kudorora na kudhoofika Marekani zinazidi kudhihirika siku baada ya siku.