Kufikichwa wanajeshi sita wa Kizayuni ndani ya saa 24 zilizopita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106482-kufikichwa_wanajeshi_sita_wa_kizayuni_ndani_ya_saa_24_zilizopita
Jumanne ya jana, jeshi la Israel lilikiri kuangamizwa askari jeshi wake sita katika saa 24 zilizopita.
(last modified 2023-12-27T04:40:59+00:00 )
Dec 27, 2023 04:40 UTC
  • Kufikichwa wanajeshi sita wa Kizayuni ndani ya saa 24 zilizopita

Jumanne ya jana, jeshi la Israel lilikiri kuangamizwa askari jeshi wake sita katika saa 24 zilizopita.

Kwa mujibu wa IRNA, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kuwa kufuatia kuendelea kuangamizwa wanajeshi wao idadi ya wanajeshi waliouawa tokea uvamizi wa nchi kavu wa Gaza imeongezeka na kufikia 161.

Wakati huo huo, Al Jazeera iliripoti Jumanne jioni, ikinukuu Jeshi la Kizayuni, kwamba askari wengine wawili wa utawala huo waliuawa jana katika operesheni ya nchi kavu huko kusini mwa Gaza na askari wengine watatu kujeruhiwa.

Tangu kuanza harakati ya Kimbunga cha Al-Aqsa, jeshi la Kizayuni kila siku limekuwa likitangaza kwa mchujo majina ya askari wake walioangamia.

Hatua hii imechukuliwa kutokana na idadi kubwa ya wanajeshi wa Kizayuni wanaoendelea kupoteza maisha na kujeruhiwa katika vita vya Gaza na hofu ya kutokea ghasia na malalamiko ya ndani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.