UNICEF: Watoto katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hali mbaya sana
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106902-unicef_watoto_katika_ukanda_wa_gaza_wanakabiliwa_na_hali_mbaya_sana
Mfuko wa Watoto waa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, hahli ya watoto katika Uukaanda wa Gaza ni mbaya mno.
(last modified 2024-01-07T04:31:37+00:00 )
Jan 07, 2024 04:31 UTC
  • UNICEF: Watoto katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hali mbaya sana

Mfuko wa Watoto waa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, hahli ya watoto katika Uukaanda wa Gaza ni mbaya mno.

Katika ripoti yake kuhusu hali ya watoto katika Ukanda wa Gaza, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetahadharisha kuwa kuenea kwa migogoro, utapiamlo na kuongezeka kwa magonjwa huko Gaza kumeleta hali mbaya katika eneo hili.

Katika ripoti yake hiyo, UNICEF imeashiria umaskini uliokithiri wa chakula wa asilimia 90 ya watoto walio chini ya umri wa miaka miwili huko Gaza.

Aidha ripoti ya UNICEF inasema: Zaidi ya watoto milioni moja huko Gaza wako hatarini kiafya.

Watoto ni wahanga wakuu wa hujuma na mashambulio ya anga ya utawala haramu wa Israael katika Ukanda wa Gaza

 

Wiki mbili zilizopita, Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa, takriban watoto elfu moja walio chini ya umri wa miaka mitano huko Gaza wanaweza kufa kutokana na utapiamlo.

Hivi karibuni, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini alisema, idadi ya watoto Wapalestina waliouliwa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mwaka uliopita (2023) huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Baitul Muqaddas Mashariki ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa kila mwaka katika eneo hilo.

Inaelezwa kuwa, watoto wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Baitul Muqaddas Mashariki, wamekuwa wakikumbwa na ukatili kwa miaka mingi, lakini nguvu ya ukatili huo imeongezeka sana tangu mashambulizi ya Oktoba 7.