HAMAS: Tumeangamiza askari 12 wa Israel katika 'operesheni tata' Jabalia, Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i111822
Izzuddin-al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa wapiganaji wake wamewaangamiza wanajeshi 12 wa Israel katika eneo lililozingirwa la kaskazini mwa Ghaza.
(last modified 2025-08-04T11:02:59+00:00 )
May 16, 2024 07:25 UTC
  • HAMAS: Tumeangamiza askari 12 wa Israel katika 'operesheni tata' Jabalia, Ghaza

Izzuddin-al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa wapiganaji wake wamewaangamiza wanajeshi 12 wa Israel katika eneo lililozingirwa la kaskazini mwa Ghaza.

Taarifa iliyotolewa na Al-Qassam hapo jana imesema, katika operesheni tata iliyotekelezwa katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza, wapiganaji wa Al-Qassam walilenga buldoza la kijeshi la Israel aina ya D9 kwa kombora la Yassin 105 na kuwalenga pia wanajeshi wa Kizayuni waliokuwa wamejificha ndani ya nyumba moja kwa makombora mawili na kupambana nao.
 
Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa, mara baada ya kikosi cha uokoaji cha jeshi la Kizayuni kukaribia eneo hilo, wapiganaji wa Al-Qassam waliripua mada za miripuko walizotega kwenye kifaru cha adui aina ya Merkava kilichokuwepo hapo, na baada ya hatua ya kujaribu kukiondoa kifaru hicho cha kikosi cha uokoaji kilichotumwa eneo hilo jeshi la anga la Israel liliripua kikatili na kiholela eneo hilo, na wapiganaji wa al-Qassam wamethibitisha kuuawa wanajeshi wasiopungua 12 wa Israel katika operesheni hiyo.
Askari kadhaa wa Kizayuni walioangamizwa vitani licha ya ufichaji habari wa Wazayuni

Wakati huohuo, Brigedi za Abu Ali Mustafa, kundi jingine la Muqawama la Palestina, limetangaza kuwa limefanya shambulio la roketi lililolenga vikosi vya jeshi la Kizayuni mashariki mwa kambi ya Jabalia.

Kundi la brigedi ya Nasser Salahuddin nalo pia limetangaza kuwa katika operesheni ya pamoja na vikosi vya al-Qassam, wameripua gari la kijeshi la askari wa jeshi la Kizayuni kwa bomu nata na kwamba askari waliokuwemo ndani yake wameuawa au kujeruhiwa.

Katika taarifa nyingine, kundi hilo limetangaza kuwa katika operesheni ya pamoja na Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina, limeshambulia eneo la walowezi wa Kizayuni wa Sdirut karibu na Ukanda wa Ghaza kwa makombora 2 aina ya 107.../