Mufti wa Oman awataka Waislamu kuwapatia wakazi wa Gaza chakula na silaha
(last modified Tue, 16 Jul 2024 11:36:44 GMT )
Jul 16, 2024 11:36 UTC
  • Mufti wa Oman awataka Waislamu kuwapatia wakazi wa Gaza chakula na silaha

Mufti Mkuu wa Oman amewataka Waislamu wote kutumia sehemu ya fedha zao kuwasiadia kwa chakula na silaha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili amesema: Tunatoa rambirambi zetu za dhati na dua zetu kwa taifa ndugu la Palestina, hususan. watu wa Gaza, katika msiba mkubwa uliosababishwa na ukatili wa utawala wa Kizayuni ulitokea katika ardhi pendwa ya Gaza na kuchukua uhai wa wanaume, wanawake na watoto pamoja na idadi kadhaa ya mateka.

Mufti wa Oman ameashiria jinai za utawala ghasibu wa Israel huko Palestina na kusema, pamoja hayo yote, lakini tuna matumaini juu ya ushindi mkubwa na wa karibu, kwa sababu hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu kkwa viumbe wake.

Karibu Wapalestina 39,000 wameuawa shahidi tangu kuanza hujuma ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7) 

 

Aidha amesema, tunawaomba Waislamu wote - hasa katika siku hizi tukufu - kutumia sehemu ya mali yao kwa ajili ya watu walioathirika wa Palestina, hasa watu wa Gaza, kutoa chakula, silaha na gharama nyingine za maisha. Kugharamia haya ni wajibu kwa kila Muislamu.

Wakati huo huo, idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7) imekaribia watu 39,000.

Uungaji mkono wa wazi wa Marekani na nchi za Magharibi umepelekea kushuhudiwa faili jeusi la viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni wanaoua watu wasio na ulinzi wala hatia. Bila shaka wale wote wanaohami na kuunga mkono jinai za Israel wanahusika pia katika jinai na mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.