Wazayuni waendelea kuwatia mbaroni raia wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11416-wazayuni_waendelea_kuwatia_mbaroni_raia_wa_palestina
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameyashambulia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds inayokaliwa kwa mabavu na kisha kuwatia mbaroni raia kadhaa wa Kipalestina.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 17, 2016 07:54 UTC
  • Wazayuni waendelea kuwatia mbaroni raia wa Palestina

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameyashambulia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds inayokaliwa kwa mabavu na kisha kuwatia mbaroni raia kadhaa wa Kipalestina.

Wanajeshi wa Israel leo asubuhi waliushambulia mji wa al Khalil kusini mwa Ukingo wa Magharibi na kuwakamata mateka Wapalestina watatu katika kitongoji cha Bait-Awa.

Wanajeshi wa Israel pia wamewatia mbaroni raia wengine wawil wa Palestina katika kitongoji cha Samuu huko al Khalik na kuwapeleka kusikojulikana.

Katika upande mwingine maghasibu wa Kizayuni wameishambulia kambi ya Qalandiya huko Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuwatia nguvuni vijana kadhaa wa Kipalestina.