Vladimir Putin atahadharisha kuhusu hali mbaya ya Asia Magharibi
(last modified Thu, 25 Jul 2024 11:20:23 GMT )
Jul 25, 2024 11:20 UTC
  • Vladimir Putin atahadharisha kuhusu hali mbaya ya Asia Magharibi

Rais Vladimir Putin wa Russia ametahadharisha kuhusu hali inayozidi kutokota ya eneo la Magharibi mwa Asia.

Rais wa Russia Vladimir Putin aliyasema hayo jana jioni, mjini Moscow katika mazungumzo yake na mwenzake wa Syria, Bashar al-Assad, katika ziara ambayo haijatangazwa ya kiongozi huyo wa Syria, ambayo ilijadili uwezekano wa kufanyika mkutano wa kilele baina ya viongozi waUturuki na Syria.

Taarifa iliyotolewa na Kremlin mapema leo, ambayo iliambatanishwa na kipande cha video cha mkutano huo, imesema Putin na Assad wamejadili suala la kuongezeka kwa mivutano katika Mashariki ya Kati kutokana na vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza. 

Putin amesema: Kwa bahati mbaya, hali katika Asia Magharibi inazidi kuwa mbaya; vivyo hivyo huko Syria. Vilevile ametilia mkazo udharura wa kuimarishwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya Moscow na Damascus.

Kwa upande wake, Rais wa Syria Bashar Assad amesema kwamba Russia na Syria zimepita kwenye majaribio magumu sana katika miongo kadhaa iliyopita na kushuhudia michakato tata ya mabadiliko. Amesema: Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendeleza kiwango cha kuaiminiana kwa pande mbili na kwamba suala hilo linaonyesha ukomavu wa watu wa nchi mbili hizo. 

Shirika la bahari la Reuters limenukuu duru za Kremlin kwamba viongozi hao wawili wamejadili maswala mbalimbali yanayohusiana na Mashariki ya Kati, pamoja na uwezekano wa kufanyika mkutano kati ya Assad na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Uhusiano wa pande mbili ulikatwa kwa zaidi ya miaka 10 sasa baada ya Syria kuituhumu Uturuki kuwa iliwaunga mkono na kuwasaidia wapiganaji wa Daesh na makundi ya kitakfiri.