Sep 07, 2024 07:18 UTC
  • Mamilioni ya Wayamen waandamana kuunga mkono msikiti wa al-Aqswa

Mamilioni ya wananchi wa Yemen wameandamana katika mji mkuu Sana’a na katika majimbo kadhaa siku wakitangaza himaya na uungaji mkono wao kwa msikiti wa al-Aqswa.

Ripoti zinaeleza kuwa, kwa mara nyingine tena mamilioni ya wananchi wa Yemen wamemiminika barabarani kulaani jinai za utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.

Mbali na San'a mikoa mingine kulikofanyika maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen ni pamoja na Sa'ada, Ma'rib na mikoa mengine kama ya Umran, Aab, Taiz, Dhamar, n.k.

Waandamanaji hao wamepiga nara za kulaani hujuma na mashambulio ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel katika ukanda wa Gaza.

Wakiwa wamebeba mabango na maberamu yenye jumbe mbalimbali waandamanaji hao wameyataja mauaji ya Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Gaza kuwa ni "uhalifu wa karne."

Maandamano ya kuunga mkono Palestina

 

Kadhalika waandamanaji hao wametangaza  mshikamano wao na watu wa Palestina wanaokabiliwa na mashambulizi ya anga na mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel.

Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa Marekani na nchi za Magharibi, utawala ghasibu wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina.