Ndege zisizo na rubani za Hizbullah (Hud-hud) zachukua tena picha na video za vituo muhimu vya Israel
(last modified Thu, 10 Oct 2024 08:00:27 GMT )
Oct 10, 2024 08:00 UTC
  • Hud-hud ikichukua picha na video za vituo muhimu vya Israel
    Hud-hud ikichukua picha na video za vituo muhimu vya Israel

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeonyesha picha na video za vituo muhimu vya kijeshi, makao makuu, na maeneo ya kistatijia ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Haifa-Carmel, zilizochukuliwa na ndege zake zisizo na rubani za harakati hiyo zinazojulikana kwa jina la Hud-hud.

Picha hizo zinaonyesha kwa kina maeneo nyeti na muhimu sana ya Haifa-Karmel ambayo yanaounda ukanda wa kwanza wa kistratijia wa ulinzi wa vitongoji vya jiji la Tel Aviv.

Picha na video hizo za Hizbullah pia zinaonyesha wazi maeneo ya viwanda, vituo vya kusafisha mafuta pamoja na idadi kadhaa ya vituo vya mawasiliano vya kijeshi huko Haifa.

Eneo hilo lilipogigwa picha na drone za Hizbullah pia lina mitambo kadhaa ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na rada ya Iron Dome, pamoja na vituo muhimu sana vya viwanda, utalii na masuala ya kisayansi.

Drone za Hod-hud zimechukua video na picha ya maeneo ya kistatijia ya Israel

Miongoni mwa shabaha zilizofuatiliwa na kupigwa picha na video na ndege zisizo na rubani za Hizbullah ni maeneo ya mfumo wa Iron Dome, wenye jukumu la kukabiliana na makombora, pamoja na mitandao ya mahandaki na barabara za chini ya ardhi, zinazotumiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kama hospitali mbadala, iwapo mji huo utapigwa kwa bomu. 

Awali Hizbullah ilitoa taarifa Jumanne wiki hii, ikitishia kuigeuza Haifa na kuifanya kama eneo la Kiryat Shmona, kwenye mpaka na Lebanon, lililokimbiwa na walowezi kutokana na ukali wa makombora ya harakati hiyo ya mapambano.