Feb 14, 2016 01:54 UTC
  • Zarif: Wasyria wenyewe waamue mustakabali wao

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa uamuzi juu ya serikali ijayo ya Syria uko mikononi mwa wananchi wa nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi habari kabla ya kuondoka Ujerumani akirudi nyumbani hiyo jana, Muhammad Javad Zarif alijibu matamshi ya Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akisema: Uamuzi kuhusu mustakbali wa Rais Bashar Assad wa Syria umo mikononi mwa Wasyria wenyewe. Zarif ameongeza kuwa, inawezekana kufikia mapatano ya kisiasa na Rais Assad na kusema kuwa, hakuna nchi yenye haki ya kuzungumzia suala la serikali ijayo nchini Syria na ni Wasyria pekee ndio wanaoweza kuchukua uamuzi kuhusu suala hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikuwa mjini Munich, Ujerumani alikoshiriki mkutano uliohusu Syria ambako kulifikiwa mapatano ya kusitisha mapigno nchini humo. Mkutano wa 52 wa Amani wa Munich ulioanza tarehe 12 hadi 14 Februari ulihudhuriwa na viongozi wa nchi 23 na makumi ya mawaziri wa mambo ya nchi za nje.

Tags