Al Mayadeen: Wanajeshi wa Ukraine wanashirikiana na magaidi huko Syria
(last modified Tue, 03 Dec 2024 12:12:15 GMT )
Dec 03, 2024 12:12 UTC
  • Al Mayadeen: Wanajeshi wa Ukraine wanashirikiana na magaidi huko Syria

Duru za habari za Syria zimetangaza kuwa wanajeshi wa Ukraine wanashirikiana na magaidi dhidi ya serikali ya syria.

Televisheni ya al Mayadeen imezinukuu duru za habari za Syria na kuarifu kuwa wanajeshi wa Ukraine wapo nchini Syria ili kushirikiana na kundi la kigaidi la Jabhatu Nusra huko Halab, kaskazini magharibi mwa Syria. 

Duru moja ya Syria pia imearifu kuwa, magaidi wa kundi la Jabhatu Nusra limeushambulia mji wa Halab kwa kushirikiana na Ukraine na Marekani. 

Makundi ya kigaidi yamefanya mashambulizi makubwa tangu Novemba 27 mwaka huu katika kambi za kijeshi za jeshi la Syria katika maeneo ya kaskazini magharibi, magharibi na kusini magharibi mwa mji wa Halab kwa kusaidiwa na baadhi ya nchi na mamluki ajinabi waliowasili huko Syria.

Jeshi la Syria pia siku kadhaa zilizopita limejibu hujuma za magaidi na kuyashambulia maeneo yanayoshikiliwa na magaidi nchini humo kwa kuungwa mkono na kikosi cha anga cha Russia.  

Vikosi vya jeshi la Syria