Ndege za Saudia zaendelea kuua watoto Yemen
(last modified Tue, 02 Aug 2016 07:22:39 GMT )
Aug 02, 2016 07:22 UTC
  • Ndege za Saudia zaendelea kuua watoto Yemen

Watoto watatu wa familia moja wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia katika maeneo ya raia kusini mwa Yemen.

Kanali ya televisheni ya al-Masirah ya Yemen imeripoti kuwa, mapema leo ndege hizo za kijeshi za Aal-Saud zimefanya mashambulizi ya anga na kulenga majengo ya raia katika kijiji cha al-Shamil, wilaya ya Wuday mkoani Abyan na kuua watoto watatu na kujeruhi vibaya wazazi wao.

Watoto ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya anga ya Saudia nchini Yemen

Wakati huohuo, askari wa jeshi la wananchi wa Yemen wametekeleza hujuma ya kulipiza kisasi kwa kuishambulia kwa maroketi kambi ya jeshi ya Saudia ya Ma'azab katika eneo la Jizan, kusini magharibi mwa nchi. Aidha wanajeshi hao wa kujitolea wameishambulia kambi ya jeshi ya Aal-Saud katika mji wa Sababa katika eneo hilo hilo.

Ndege za kivita za Saudia

Ni karibu mwaka mmoja na nusu sasa Saudia ikishirkiana na muungano wake bandia wa kijeshi imeizingira na kuishambulia Yemen kutokea angani na ardhini kwa kisingizio cha kutaka kuirejesha ile utawala wa Aal Saud unayoiita serikali 'halali' ya Abd Rabbuh Mansur Hadi.

Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulio hayo na taasisi nyingi za miundombinu ya nchi hiyo masikini zimeteketezwa bila ya watawala wa Aal Saudi kufikia malengo yao yasiyo ya kibinadamu.