Waandamanaji Tel Aviv watishia kumuua Netanyahu
(last modified Sun, 27 Apr 2025 13:15:37 GMT )
Apr 27, 2025 13:15 UTC
  • Waandamanaji Tel Aviv watishia kumuua Netanyahu

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ameendelea kuandamwa na mashinikizo baada ya kufanyika maandamano mengine dhidi yake huku waandamanaji wakitishia kumuua.

Maandamano kwenye mtaa wa Kaplan mjini Tel Aviv na kuonyeshwa "vichwa vilivyokatwa" na hivyo kutishia kumuua Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, yamekikasirisha chama cha Likud. Chama hicho kimemshambulia mkuu wa usalama wa ndani (Shabak) na mwanasheria mkuu wa Israel, kikitaka waandamanaji wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.

Katika ripoti yake, kanali ya televisheni ya Kanali 12 ya Israel imeeleza kuwa, katika maandamano hayo jana jioni (Jumamosi) ya wapinzani wa Netanyahu kwenye mtaa wa Kaplan wa Tel Aviv, waandamanaji walionyesha picha ya vichwa vilivyokatwa mithili ya Benjamin Netanyahu kwenye suala ambalo limekikasirisha chama cha Likud.

Kwa mujibu wa ripoti ya chombo hicho cha habari cha Kizayuni, wanachama wa Likud, ambao Netanyahu ndiye kiongozi wao, wamesema kuwa, kuonyeshwa kwa vichwa vilivyokatwa na waandamanaji ni uchochezi na tishio la kumuua Waziri Mkuu wa Israel, na katika majibu makali, walimshambulia, mkuu wa huduma ya usalama wa ndani (Shabak) na Mwendesha Mashtaka aliyeko katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huo huo, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni yanaonesha kuwa, Wazayuni walio wengi wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) wanasema kuwa Netanyahu anapaswa kujiuzulu na kukubali kubeba jukumu la kushindwa mkabala wa oparesheni ya wanamapambano wa Palestina ya tarehe 7 Oktoba mwaka 2023.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, akthari ya Wazayuni wanaoishi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) wanaamini kuwa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo anapasa kujiuzulu na kubeba dhima ya matukio ya Oktoba 7.